ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUZA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUZA' (/showthread.php?tid=2398) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUZA' - MwlMaeda - 02-12-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUZA' Neno *ajuza* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino [Ngeli: a-/wa- wingi: maajuzi]* yenye maana mtu wa jinsi ya kike aliyezeeka sana; mwanamke aliyekonga sana. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ajuza*( *soma: ajuuzatun/ajuuzatan/ajuuzatin عجوزة )* limetamatishwa na herufi ya Kiarabu taau (t ة) ya mkunjo ambayo ni alama ya jina la kike ingawa katika lugha ya Kiarabu neno hili hutumika bila ya hiyo herufi (t ة) yaani: *ajuuzun/ajuuzan/ajuuzin عجوز* kwa mwanamume na mwanamke. Neno hili linatokana na *kitenzi* cha Kiarabu *ajaza عجز* chenye maana: ameshindwa. Neno *ajuuzun* (soma: *ajuuzun/ajuuzan/ajuuzin عجوز* ) katika lugha ya Kiarabu lina maana zifuatazo: 1. Mtu wa jinsi ya kike au kiume aliyezeeka. Huitwa pia *harimu هرم* . 2. Siku za baridi kali *ayyaamul ajuuzi أيام العجوز* katika msimu wa baridi ambazo ni siku saba: siku nne za mwisho wa mwezi *Februari* na siku tatu za mwanzo wa mwezi *Machi* . 3. Pombe. 4. Ardhi. 5. Simba 6. Mbwa mwitu. 7. Sungura. 8 . Ng'ombe jike. 9 . Ngamia jike. 10 . Sindano. 11 . Kisima. 12 . Bahari. 13 . Shujaa 14 . Mfanyabiashara. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *ajuuzun/ajuuzan/ajuuzin عجوز* llilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ajuza* Waswahili walichukua maana moja tu ya mtu aliyekonga na wakamhusisha mtu wa jinsi ya kike tu na kumuacha mtu wa jinsi ya kiume kama walivyoziacha maana nyingine 13 za neno hili katika lugha ya Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |