MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JE, NI KWELI KISWAHILI KILIZALIWA ZANZIBAR? - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
JE, NI KWELI KISWAHILI KILIZALIWA ZANZIBAR? - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: JE, NI KWELI KISWAHILI KILIZALIWA ZANZIBAR? (/showthread.php?tid=2390)

JE, NI KWELI KISWAHILI KILIZALIWA ZANZIBAR? - MwlMaeda - 02-06-2022

Jee Ni Kweli Kiswahili Kilizaliwa Zanzibar?
Hakika ilikuwa ni furaha kubwa kuona shamra shamra za Tuzo za Kiswahili jijini Dar-es-Salaam – Tazama Video - kibonyezi kiko tini ya ujumbe huu. Na kwa kupata Waziri Mkuu katika sherehe kama hii ni jambo la kutia moyo sana! Naomba tuzo hizi, tini ya uongozi wa wapenzi wa Kiswahili mbali mbali ulimwenguni, zitaendelea kukikuza Kiswahili na Fasihi yake.
Mbali na hayo, baina ya dakika ya ishirini na mbili (22) na dakika ya ishirini na nne (24) ya video hii, Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Kassim Majaliwa, amesema jambo ambalo limenistaajabisha mno! Amesema,
“… Kwetu Tanzania ambako Kiswahili ndiyo kilizaliwa. … Kiswahili kilizaliwa Zanzibar, kikahamia bara, kikasambaa nchini Kenya. …"
Kusema kweli historia hii ya Kiswahili nlikuwa siijui! Mimi siku zote nikidhania hichi Kiswahili chanzo chake ni Kingozi, na nikidhania Kingozi shina lake liko katika maeneo yalioko kwenye Mwambao wa (au Pwani ya) nti tuijuayo leo kama Kenya – yaani miji kama vile Lamu, Mambasa, na Vanga. Sasa leo kusikia kuwa Kiswahili, hata kabla ya kufika Pwani ya Kenya kilipita “Tanzania bara” (Tanganyika) kwanza, nimeshangazwa mno!
Katika magwiji au wataalamu wa lugha ya Kiswahili niliowasiliana nao na kuwauliza ikiwa ni kweli kuwa Kiswahili kilizaliwa Zanzibar? Mmoja alinambia kuwa,
“Hapana ushuhuda wa aina yoyote kwamba Kiswahili 'kilizaliwa Zanzibar.' Hayo yaliosemwa ni maoni yasiyokuwa na msingi.” 
Na wa pili alisema kuwa, 
“Si kweli! Hayo si maoni yaliyotokana na utafiti wa kitaaluma wala hayakubaliani na ushahidi wa kihistoria.”
Khatari ninayoiona mimi ni kuwa jambo kama hili likiwa limesemwa na mtu mwenye wadhifa mkubwa sana kama huo, kwenye nchi yenye kukipenda na kukikuza Kiswahili kama Tanzania, basi huenda likaishilia kwenye vitabu vya shule, na wanafunzi (na raia) wataanza kusoma jambo hilo na hatimae litatukuliwa kuwa ni “kweli” ambayo itakuwa ni vigumu kui-challenge katika miaka ijayo.
Mimi nadhani pana umuhimu wa riwaya hii ya kiongozi wetu huyu mpendwa (na hakika nampenda yeye Waziri Mkuu na nampenda sana Raisi wa Tanzania) kuwa-challenged sasa kabla ya jambo hilo halijamea mizizi! Ndia moja ya kuli-challenge jambo hili ni watu wenye kuheshimika katika lugha ya Kiswahili kuandika makala (Op-ed) kwenye magazeti ya Tanzania na Kenya (na piya kwenye mihadhara na kwenye vyombo vyingine vya khabari) kuyasahihisha maneno hayo ya Waziri Mkuu na kusema kuwa tunakhitilafiana nayo kwa sababu hii na hii na hii. Yaani, ni muhimu ijulikane wazi kuwa kuna watu hawakubaliani kabisa na riwaya hiyo.
Kwanza wa-Zanzibari ndiyo walipata fursa ya lahaja yao kutumiwa kama “Standard” Kiswahili. Na pili leo tumeanza “kuelimishwa” kuwa Kiswahili kimeanza huko piya! Mimi sina vita na watu wa Zanzibar, na ukitaka kweli ni kuwa ni watu ninaowapenda sana kwenye dhati ya nafsi yangu na ni watu niloingiliana nao kwa damu na mahabba makubwa. Lakini piya ni mtu ambaye napenda haki na ukweli; na napenda haki na ukweli zidumishwe. Na ikiwa hatutovidumisha hivi basi sote tutakuwa mas-ulia kwa vizazi vijavyo kwa kunyamaa kimya kwa kupotolewa historia ya lugha yetu.
Na yawezekana sana kuwa Waziri Mkuu hakukusudia kuipotoa historia bali ni kutojuwa kwake tu. Kwa hivyo upo umuhimu aelezwe kwa ndia ya heshima na adabu kuwa hayo aliyoyasema ni “maoni yasiyokuwa na msingi” na “si maoni yaliyotokana na utafiti wa kitaaluma wala hayakubaliani na ushahidi wa kihistoria.”
Na ni matumaini yangu kuwa atakapoelezwa haya Waziri Mkuu (na wengineo wenye maoni kama hayo), wataweza kukubali makosa yao.
Natumai mutayasambaza makala haya kwa wapenzi wa Kiswahili na kwenye makundi ya Kiswahili yaliopo kwenye vyombo kama vya Facebook, WhatsApp, Telegram, na piya kwenye idara za Kiswahili za vyombo vya Khabari (Televisheni, maredio, na magazeti), na za Vyuo Vikuu vilioko Tanzania, Kenya, na nchi nyinginezo.
Ahsanteni sana.
Ndugu Yenu,
Muhammad bin Yusuf