ETIMOLOJIA YA MANENO 'AJILA' NA 'AJILANI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'AJILA' NA 'AJILANI' (/showthread.php?tid=2389) |
ETIMOLOJIA YA MANENO 'AJILA' NA 'AJILANI' - MwlMaeda - 02-05-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'AJILA' NA 'AJILANI' Neno *ajila* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* hali ya kufanya kitu kwa haraka; fanya jambo himahima. 2. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* utendaji jambo bila kukawia. 3. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* umuhimu. Katika lugha ya Kiarabu, neno *ajila* limekopwa kutoka nomino ya Kiarabu *aajilun/aajilan/aajilin عاجل* yenye maana zifuatazo: 1. Mwenye kufanya haraka. 2. Hali ya kutokea jambo kwa haraka. 3. Jina lingine la dunia; mahali pa kupita kwa haraka. Neno *ajilani* katika lugha ya Kiswahili ni kielezi chenye maana ya bila kukawia, mara moja, hivi sasa. Katika lugha ya Kiarabu, neno *ajilani* limekopwa kutoka nomino ya Kiarabu *ajlaanu/ajlaana عجلان* yenye maana zifuatazo: 1. Mwenye kufanya mambo yake haraka haraka. 2. Mwenye kutembea kwa haraka kuwahi shughuli zake. Kinachodhihiri ni kuwa maneno *ajila* na *ajilani* yalipokopwa kutoka Kiarabu hayakuacha maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu isipokuwa Waswahili waliliweka neno *ajilani* katika kategori mpya - *kielezi* na kulipa neno *ajila* maana mpya - umuhimu *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |