ETIMOLOJIA YA NENO 'RAKADHA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'RAKADHA' (/showthread.php?tid=2306) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'RAKADHA' - MwlMaeda - 01-26-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'RAKADHA' Neno rakadha katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo: 1. Hali ya kung'ang'ania jambo: Fanyia rakadha. 2. Ulazima wa/shurutisho la kukamilisha jambo. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili rakadha( soma: rakadhwa ركض ) ni kitenzi cha Kiarabu chenye maana zifuatazo: 1. Amekwenda mbio. 2. Amekita mguu chini. 3. Ametetea. 4. Amempiga mnyama mbavuni ili kumuhimiza aongeze mwendo. 5. Amerusha mshale. 6. Nyota zimetembea angani. 7. Ndege amepigapiga mabawa yake. 8. Amekimbia. Kinachodhihiri ni kuwa kitenzi cha Kiarabu rakadhwa ركض kilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa nomino ya Kiswahili ' rakadha ' lilibeba maana mpya ya hali ya kung'ang'ania jambo na ulazima wa/shurutisho la kukamilisha jambo. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |