MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHI/AKHI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHI/AKHI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHI/AKHI' (/showthread.php?tid=2265)

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHI/AKHI' - MwlMaeda - 01-20-2022

Neno ahi/akhi katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/-wa] yenye maana ya:

1. Ndugu wa kiume; kaka.

2. Mwenzako wa karibu.

3. Mtu mwenye mapato duni, mtu wa kipato kidogo;  asiye na chochote.

4. Mtu mwenye uhusiano nawe kama vile ndugu wa kuzaliwa, rafiki, mpenzi, mke au mume.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ahi/akhi( soma: akhun/akhan/,akhin اخ ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo

1. Ndugu wa kuzaliwa kwa baba na mama.

2. Rafiki.

3. Daraja la baadhi ya viongozi wa dini ya Uyahudi ambao hawajafikia daraja la ukuhani.

4. Jina wanaloitana Wajenzi Huru 'Albannaauuna Al-Ahraa' Freemasons.

5. Mwenza katika kazi aghalabu hutumiwa na wanajeshi.

6. Sauti inayoashiria maumivu au ghadhabu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili akhun lilipoingia katika  Kiswahili na kutoholewa kuwa ahi/akhi lilichukua kutoka lugha ya asili - Kiarabu maana ya uhusiano wa kidugu na urafiki wa karibu na likaongeza maana mpya ya mtu mwenye mapato duni; asiye na  chochote.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.