ETIMOLOJIA YA NENO 'AHERA/AKHERA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AHERA/AKHERA' (/showthread.php?tid=2247) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AHERA/AKHERA' - MwlMaeda - 01-18-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHERA/AKHERA' Neno *ahera/akhera* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/-zi*] yenye maana ya: 1. Mahali panapoaminiwa kuwa ndiko roho za wafu zinakoenda. 2. Maskani ya roho za wanadamu baada ya mauti/kifo. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ahera/akhera*( *soma: aakhiratun/aakhiratan/,aakhiratin آخرة )* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Kinyume cha Dunia. Kuna aya katika Qur'aan Tukufu isemayo: "Miongoni mwenu wapo wanaoitaka Dunia, na miongoni mwenu wapo wanaoitaka Akhera." (Qur'aan Tukufu, Sura ya 3 (Surat Aali Imraan, Aya ya 152). 2. Kinyume cha mwanzoni; mwishoni. 3. Maskani ya roho za wanadamu baada ya kifo. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *aakhira* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa limezoeleka kutamkwa *ahera* na *akhera* likibeba maana moja ya maskani ya roho za wanadamu baada ya kifo. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |