MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AHSANTE' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'AHSANTE' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AHSANTE' (/showthread.php?tid=2238)

ETIMOLOJIA YA NENO 'AHSANTE' - MwlMaeda - 01-17-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHSANTE'

Neno ahsante katika lugha ya Kiswahili ni kihisishi: tamko analotoa mtu wakati wa kushukuru.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ahsante( soma: ahsanta/ahsanti/ahsantumaa/ahsantum/ahsantunna ) احسنت/احسنتما/احسنتم/احسنتن) ni kitenzi cha Kiarabu chenye maana ya kufanya vizuri.
Ahsanta = Wewe mwanamume umefanya vizuri.
Ahsanti = Wewe mwanamke umefanya vizuri.
Ahsantumaa = Nyinyi wawili mmefanya vizuri.
Ahsantum = Nyinyi wanaume wengi mmefanya vizuri.
Ahsantunna = Nyinyi wanawake wengi mmefanya vizuri.

Neno hili, kwa wazungumzaji wa pwani, wamezoea kulichukua kama lilivyo katika Kiarabu kwa  mwanamume mmoja kumwambia ahsanta , mwanamke mmoja kumwambia ahsanti , watu wawili kuwaambia ahsantumaa , wanaume wengi kuwaambia ahsantum , na wanawake wengi kuwaambia ahsantunna.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ahsante ambalo hutumika bila ya kuzingatia jinsia, ambalo kwa watu wengi huwa ahsanteni, halikutumika sana kwa Waswahili wa pwani ambao walizowea kulitumia kama linavyotumika katika lugha ya Kiarabu. 

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.