ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADI' (/showthread.php?tid=2222) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADI' - MwlMaeda - 01-14-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADI' Neno ahadi katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. Nomino: [Ngeli: i-/-zi] mwisho wa uhai wa kiumbe aghalabu mwanadamu; mauti. 2 - Nomino: [Ngeli: i-/-zi] makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande mbili au zaidi. 3 - Nomino: [Ngeli: i-/-zi] hakikisho la utekelezaji wa jambo ambalo mtu au watu hujipa jukumu la kutimiza. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ahadi( soma: ahdun/ahdan/ahdin عهد ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Ahadi : tendo-jina kutokana na kitenzi cha Kiarabu ahida عهد ameahidi. 2. Utekelezaji wa jambo fulani. 3. Dhamana. 4. Amani. 5. Mapenzi. 6. Dhima. 7. Azimio; makubaliano. 8. Wasia/wosia, usia. 9. Kiapo. 10. Andiko la uhawilishaji wa madaraka. 11. Zama/wakati, ahdush shabaabi عهد الشباب wakati wa ujana. 12. Mrithi wa ufalme, ikitanguliwa na neno waliyuu, waliyyul Ahdi ولي العهد. 13 - Agano la Kale, likiambatana na neno Al-Qadiim, Al-Ahdul Qadiim العهد القديم، maandiko matakatifu kabla ya ujio wa Masihi Issa Mwana wa Maryam (Yesu Kristo). 14 - Agano la Jipya, likiambatana na neno Al-Jadiid, Al-Ahdul Jadiid العهد الجديد، maandiko matakatifu yanayohusu wakati wa Masihi Issa Mwana wa Maryam (Yesu). Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ahadi ( soma: ahdun/ahdan/ahdin عهد ) lilipoingia katika Kiswahili lilichukua baadhi ya maana zake katika lugha ya asili- Kiarabu na kuacha maana zingine. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |