UFAHAMU NA UFUPISHO (ZOEZI) - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sekondari (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=4) +---- Forum: Kidato cha nne (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=40) +----- Forum: Mitihani (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=42) +----- Thread: UFAHAMU NA UFUPISHO (ZOEZI) (/showthread.php?tid=21) |
UFAHAMU NA UFUPISHO (ZOEZI) - MwlMaeda - 06-15-2021 Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata Niliendelea mbele kidogo, nikasema, nikatazama kulia, kushoto, mbele nyuma halafu kushoto tena, huku nikiwa makini zaidi. Moyo wangu uliniambia kwa huruma “cherwa, kamwe usipige hatua yoyote toka hapo ulipo na sasa tazama chini karibu na miguu yako.” Kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firaubi, niliona Joka kubwa ambalo lilikuwa limepanua mdomo wake mithili ya pango. Niligutuka ghafla na kuhamaki, nilijupa moyo nikaruka kuelekea nyuma, mara joka lile likageuka binti mzuri mwenye umri wa kuolewa, binti yule alinisogelea ppale nilipokuwa nisijue la kufanya. “nataka kuongea na wewe, nimetoka mbali kwa ajili yako, leo matatizo yako yataisha” alisema binti yule aliyeonekana mwenye furaha na huruma kuu pale nilipokuwa nimesimama sikujua kuwa ninabubujikwa na machozi. “nasema tulia, usilie uwe na matumaini sauti ya msichana iliingia masikioni mwangu kama vile radi au upepo uvumao kwa nguvu.
Palepale nilianguka, giza likaniteka na nikapoteza fahamu palepale mtoni, nilizinduka na kugundua kuwa nilikuwa mikononi mwa watu nisiowafahamu nikiwa nimevalishwa kanzu nyeupe, niliangalia saa katika simu yangu ilikuwa ni saa tisa na nusu usiku. Sikutambua nilipokuwa lakini niligundua kuwa pale ni msituni, mara ikasikika sauti ya upole, “upo katika mikono salama, usiogope.”
Maswali
(i) Eleza maana ya maneno/tungo zilizopigiwa mstari
(ii) Kwa nini muhusika anasema alijipa moyo?
(iii) Msichana aliyemtokea muhusika alikuwa ametoka wapi?
(iv) Muhusika alipopoteza fahamu alikuwa katika mazingira gani?
(v) Andika kichwa cha habari hii kwa maneno yasiyozidi matano.2. Fupisha habari hiyo kwa (1/3)
|