MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI:BUNDI PELEKA SALAMU - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI:BUNDI PELEKA SALAMU - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI:BUNDI PELEKA SALAMU (/showthread.php?tid=2079)

SHAIRI:BUNDI PELEKA SALAMU - MwlMaeda - 01-10-2022

Bundi peleka salamu,kwamwambie Hudihudi,
M’bainishe kalamu,mwambie si usitadi,
Asijitie wazimu,majungu siyo mradi,
Mwambie aseme yake,ya kwangu hayamuhusu.
Umbea yake asili,hilo ninalielewa,
Basi aseme ya kweli,sipendezwi singiziwa,
Hudihudi mfedhuli,fitini amejaliwa,
Mwambie aseme yake,ya kwangu hayamuhusu.

Kunichunguza ya kwangu,ubaya kunizulia,
Kusambaza ulimwengu,waja wajenichukia,
Nakula kwa nguvu zangu,sivyo anavyodhania,
mwambie aseme yake,ya kwangu hayamuhusu.

Kuninyoshea vidole,nyama yangu akaila,
Tanguliza yangu mbele,kunisabili madhila,
Aniita msukule,ati! Amenitawala,
Mwambie aseme yake,ya kwangu hayamuhusu.

Ijapo mimi kunguru,aseme yangu mazuri,
Anikosesha uhuru,kunisambazia ghuri,
Kizidi tamdhukuru,nitataja zake siri,
Mwambie aseme yake, ya kwangu hayamuhusu.

Ally Sufiani,
Morogoro.