ETIMOLOJIA YA NENO 'KADHIA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'KADHIA' (/showthread.php?tid=2078) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'KADHIA' - MwlMaeda - 01-10-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'KADHIA' Neno kadhia katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. Nomino: [Ngeli: i-/zi- ] jambo linalofanyika. 2. Nomino: [Ngeli: i-/zi-] tukio lililojiri. 3. Nomino: [Ngeli: i-/zi-] mkasa uliomfika mtu. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili kadhia *(soma: *qadhwiyyatu/qadhwiyyatan/qadhwiyyatin قضية ) ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Hukumu itolewayo na chombo cha kutoa maamuzi. 2. Suala linalobishaniwa na lilifikishwa kwa jaji/majaji kwa ajili ya kusikilizwa na kutolewa hukumu. 3. Mambo yanayohusu tapo maalumu katika jamii; qadhwiyyatun siyaasiyyat قضية سياسية kadhia ya kisiasa, qadhwiyyatun ijtimaaiyyat قضية اجتماعية kadhia ya kijamii, qaadhwiyatu Filistwiin قضية فلسطين kadhia ya Palestina. Kinachodhihiri ni kuwa neno kadhia (soma: *qadhwiyyatu/qadhwiyyatan/qadhwiyyatin قضية )ilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno kadhia lilibeba maana ya jumla ya tukio lililojiri au jambo linalofanyika. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |