ETIMOLOJIA YA NENO 'AMIRI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AMIRI' (/showthread.php?tid=2073) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AMIRI' - MwlMaeda - 01-09-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AMIRI' Neno amiri katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. Nomino: [Ngeli: a-/wa-, wingi: maamiri ] mtoto wa mfalme; mwana mfalme. 2. Nomino: [Ngeli: a-/wa-] kiongozi mwenye mamlaka ya kutoa amri. Mfano: kiongozi mkuu, amiri jeshi mkuu: mtu mwenye cheo kikubwa kijeshi anayetoa mwongozo kwa wanajeshi wengine walio chini yake. 2. Kitenzi si elekezi: amir.i anza kufanya jambo; anzisha ( Minyumbuliko : amiria, amirika, amirisha, amiriwa.) Katika lugha ya Kiarabu, neno hili amiri(soma: amiirun/amiiran/amiirin امير) ni nomino inayotokana na kitenzi cha Kiarabu amura أمر ameamrisha , lenye maana: mwenye kutoa amri. Maana zingine za neno (amiri) katika Kiarabu ni: 1. Mfalme 2. Mtoto wa mfalme. 3. Mtawala. 4. Mshauri. 5. Jirani. 6. Lakabu ya kiongozi wa Waislamu, amiru al-Muuminiina (soma: Amirul Muuminiina Kiongozi Mkuu wa Waislamu امير المؤمنين ). Kinachodhihiri ni kuwa neno amiiri (soma: amiirun/amiiran/amiirin امير ) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno amiri lilichukua baadhi ya maana zake kutoka Kiarabu na kuziacha maana zingine. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |