ETIMOLOJIA YA NENO 'HALMASHAURI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'HALMASHAURI' (/showthread.php?tid=2069) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'HALMASHAURI' - MwlMaeda - 01-09-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'HALMASHAURI' Neno *halmashauri* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* kikundi cha watu waliochaguliwa au kuteuliwa kufanya kazi ya kuwa watawala, watunga sheria, washauri au kuelekeza jambo fulani. 2. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* chombo cha kiutawala katika wilaya au mji. 2. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* kundi la watu waliochaguliwa au kuteuliwa kuelekeza utendaji wa shughuli fulani. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *halmashauri* ni naneno mawili ya Kiarabu yaliyowekwa pamoja; neno *ahlu* (soma: *ahlu/ahla/ahli اهل)* lenye maana ya *watu, -enye,* na neno *mashauri* (soma:*mashuuratun /mashuuratan/mashuuratin* *مشورة* ) pia *mash-wara* (soma: *mash-waratun/mash-waratan/mash-waratin مشورة)* lenye maana zifuatazo: 1. Kinachotolewa nasaha kwa rai au namna nyingine. 2. Ushauri. 3. Nasaha, muongozo. Kinachodhihiri ni kuwa maneno haya mawili *ahlu mashuurat/mash-warat* yaliipoingia katika Kiswahili na kutoholewa, neno jipya la Kiswahili *halmashauri* lilipatikana. Katika lugha ya Kiarabu neno *shuuraa شورى* linatumika kwa kisawe cha maneno *mashuurat مشورة* na *mash-warat مشورة* na hupatikana misamiati *ahlu al-shuuraa* (soma: *ahlush shuraa اهل الشورى washauri)* na *majlis al-shuuraa* (soma: *majlisush shuraa مجلس الشورى baraza la ushauri; bunge).* *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |