ETIMOLOJIA YA NENO 'AFRO' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFRO' (/showthread.php?tid=2055) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AFRO' - MwlMaeda - 01-08-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFRO' Neno *afro* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. *Kivumishi* : -enye asili ya Afrika; -a Kiafrika. 2. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* mtindo wa ufugaji wa nywele ndefu aghalabu za Kiafrika na kuzitengeneza kuwa katika umbo la kititamviringo kinachofungamana kichwa kizima. Ingawa *Kamusi Kuu ya Kiswahili* limelisajili neno hili *afro* kuwa etimolojia yake ni *Kiarabu* lakini *utafiti* nilioufanya umeonesha kuwa neno hili *(afro) si neno la Kiarabu.* Neno lenye mzizi unaoshabihiana na neno hili ni neno *frau* *فرو* lenye maana ya ngozi za wanyama zinazotumika kutengeneza nguo za kujikinga na baridi. Yapo madai kuwa neno *afro* lina asili ya *Kilatini* na wengine wamedai kuwa etimolojia yake ni *Kiingereza* . *Kinachodhihiri ni kuwa neno (afro) halina uhusiano na lugha ya Kiarabu.* *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |