ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI (/showthread.php?tid=2051) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI - MwlMaeda - 01-07-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI' Neno *afyuni* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino [Ngeli:i-/i-]* yenye maana ya 'kileo chenye umbo la kidonge kunachotengenezwa kutokana na utomvu wa *mpopi*( *afyuni* ) , ambacho kwa kawaida hutumika kama tiba ya kutuliza maumivu, aghalabu hutumiwa kinyume cha sheria kama dawa ya kulevya. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *afyuni* (soma: *afyuunun/afyuunan/afyuunib افيون)* lina maana ya 'dutu inayotolewa kwenye mpopi (afyuni) ambayo inatia ganzi na hutumiwa kwa kutuliza maumivu na kuleta usingizi, pia hutumika vibaya kama dawa ya kulevya. Kinachodhihiri ni kuwa neno *afyuni* ( *soma: afyuunun/afyuunan/afyuunin افيون*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *afyuni* halikubadili maana yake ya msingi katika lugha ya asili - Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |