ETIMOLOJIA YA NENO 'AFKANI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFKANI (/showthread.php?tid=2036) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AFKANI - MwlMaeda - 01-06-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFKANI' Neno afkani katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. Nomino: [Ngeli: a-/wa-] mtu mwenye uwezo mdogo wa akili. 2. Nomino: [Ngeli: u-/u-] ugonjwa wa moyo. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili). 3. Nomino: [i-/i-] ugonjwa wa moyo (Chanzo: Kamusi ya Karne ya 21). 4. Kivumishi: -enye wehu, -enye upungufu wa akili. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili afkani (soma: afkaanu أفكان) ni nomino inayotokana na kitenzi cha Kiarabu afika افك (افك:ضعف عقله وصار سفيها- imedhoofu akili yake na amekuwa safihi ) Kinachodhihiri ni kuwa neno afkani ( soma: afkaanu افكان) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno afkani lilichukua maana ya 'wehu' na kuacha maana zingine. Tanbihi: Kisarufi, Kamusi Kuu ya Kiswahili na ile ya Kamusi ya Karne ya 21 zimetoa ngeli mbili tofauti kulihusu neno (nomino) afkani kwa maana ya 'ugonjwa wa moyo'. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |