ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADHARAU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADHARAU (/showthread.php?tid=2030) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADHARAU - MwlMaeda - 01-05-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADHARAU' Neno *ahadharau* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino [Ngeli:i-/zi-]* yenye maana zifuatazo: 1. Rangi ya kijani. 2. Yenye rangi ya kijani kibichi. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ahadharau* si neno la Kiarabu bali ni mseto wa maneno mawili ya Kiarabu. Sarufi ya Kiarabu imeweka jinsia katika nomino, viwakilishi na vivumishi vya Kiarabu. Kwa mfano, rangi nyeupe ikikusudiwa kwa jinsia ya kiume huitwa abyadh (soma: *abyadhwu* *ابيض* ) na ikikusudiwa kwa jinsia ya kike huitwa *baydhaa* (soma: *baydhwaau* *بيضاء* ). Hivyo hivyo, rangi nyeusi itakuwa *aswadu/sawdaau* , nyekundu itakuwa *ahmaru/hamraau,* njano itakuwa *aswfaru/swafraau* na rangi ya kijani ni *akh-dhwaru* (kwa jinsia ya kiume) na *khadhw-raau* (kwa jinsia ya kike). Sasa neno *ahadharaau* ni neno jipya ambalo unaweza kulirejesha kwenye mseto wa maneno mawili ( *akhdhwaru na khadhwraau* ). Kwamba wamechukua herufi *a* katika neno *akhdhwaru* wakaliweka mwanzoni mwa neno *khadhwraau* na kupata neno jipya *akhdhwaraau* ambalo walipolitohowa kwa kuondoa herufi (k) kutoka (kh/خ) na herufi (dhw ض) wakaifanya herufi (dh/ذ) wakapata neno jipya la Kiswahili *ahadharau*. Kinachodhihiri ni kuwa neno *ahadharau* limechukua maana ya maneno *akhdhwaru* na *khadhwraau* katika lugha ya Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |