MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SHAIRI : YAZAMISHE BAHARINI MAKOSA YA MKE WAKO - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : YAZAMISHE BAHARINI MAKOSA YA MKE WAKO - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : YAZAMISHE BAHARINI MAKOSA YA MKE WAKO (/showthread.php?tid=2013)



SHAIRI : YAZAMISHE BAHARINI MAKOSA YA MKE WAKO - MwlMaeda - 01-04-2022

Kwa mapana nakusifu
hakika metakasika
mola wangu mtukufu
Wa majini malaika
Fadhila zako kunjufu
kila pahala zafika


Kwa baba wa familia
Zifike zangu salamu
Kwenye maisha ya ndoa
Changamoto na matamu
Mkeo anakosea
Hakuumbwa maasumu


yazamishe baharini
Makosa ya mke wako
Ishi nae kwa makini
Huyo ni ubavu wako
simjeruhi usoni
Kumpiga iwe mwiko


Ni bahari ya mapenzi
yenye maji kila kona
Makosa ya kipuuzi
Jifanye hujayaona
Mpe bora ya malezi
Ajisikie mwanana


Usijitie ujeshi
Ati wampa adabu
Na makosa hayaishi
Kuwa mume si sababu
Ukiwa kwao mcheshi
Kwako mwanaume gubu


Madhali sio haramu
Vikosa vya kawaida
Mpe maneno matamu
Azidi pata faida
Maneno haya fahamu
Hukumuoa kwa shida


Ebwane mke hapigwi
kwa bakora za mitini
Anapigwa kwa mahaba
Yalozama baharini
Mzamishe habahaba
Hadi aloe mwilini


Ukihisi Anajuta
Kwa alichokufanyia
Mpe mabusu matata
Huku Ukimsifia
Mwambie”kwako nadata”
“Wala hujanikosea”


Mletee vizawadi
nyumbani ukirejea
Kuwa mume maridadi
Epuka kumkemea
Atakupenda zaidi
Haya Ukizingatia


Akikosea kupika
Tena isiwe kasheshe
jitahidi kuridhika
Chakula chake ukishe
Maneno haya hakika
Jaribu uhakikishe


Mkeo akikuudhi
Usivunje wake utu
utajitia maradhi
kukosoa kila kitu
Onyesha umemridhi
kununa usithubutu


Akiichupa mipaka
Ya haramu kuyafanya
Hapo hapana mashaka
Ni lazima kumuonya
Katu sifanye dhihaka
Ni wajibu kumkanya


Akikudai talaka
Nakusihi simjibu
Ni hasira kwa hakika
zitapoa taratibu
Ukipaniki haraka
ataenda pata tabu


Ataolewa na nani?
Ukishamuacha wewe?
Aolewe na muhuni?
atajijua mwenyewe?
Na weye taoa jini?
Hakosei kama wewe?


Ukingoni nimegota
Naomba kuwasilisha
Kwa pale nilipopata
Mola kaniwafikisha
Yarabi tupe thabata
Na ndoa kuzidumisha…



Mtunzi:
Al akh Abuu hafsa