SHAIRI : BWEGE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : BWEGE (/showthread.php?tid=1943) |
SHAIRI : BWEGE - MwlMaeda - 01-03-2022 BWEGE Ni wewe ulomkubwa, ulo kipofu ni wewe Ni wewe wa sifa kubwa, mla minofu ni wewe Ni wewe bwabwabwabwa, muongofu ni wewe Ni wewe kubwajinga, mpenda sifa ni wewe. Ni wewe mwenye elimu, kushinda wote ni wewe Ni wewe mwenye walimu, sehemu zote ni wewe Ni wewe usonidhamu, mwenye akili ni wewe Ni wewe kubwajinga, mpenda sifa ni wewe. Ni wewe waturuhusu, kuvaa tupu ni wewe Ni wewe wa uchi nusu, kuuruhusu ni wewe Ni wewe inakuhusu, kesi hii ni wewe Ni wewe kubwajinga, mpenda sifa ni wewe. Ni wewe ulosharifu, mpendwa sana ni wewe Ni wewe mwongoza safu, msemwa sana ni wewe Ni wewe mwenye uchafu, ulo msafi ni wewe Ni wewe kubwajinga, mpenda sifa ni wewe. Ni wewe mwenye sheria, katika mengi ni wewe Washindwa kuitumia, kwenye msingi ni wewe Ni wewe wa ndoto mia, kuzitimiza ni wewe Ni wewe kubwajinga, mpenda sifa ni wewe. Ni wewe kwanza kuzawa, kimataifa ni wewe Ni wewe mekuwa bwabwa, sheria bubu ni wewe Ni wewe waamuliwa, na watotowo ni wewe Ama kweli kubwajinga, ni wewe mpenda sifa. Watoto wajivalia watakavyo, kimya mekaa ni wewe Watoto wazini hovyo, unatazama ni wewe Uhuria huu hovyo, weka sheria ni wewe Ni wewe kubwajinga, mpenda sifa ni wewe. Eti kichwa cha famili, na koo kubwa ni wewe Ni wewe dhoofu hali, jitu zima hovyo wewe Mabaya kwako halali, jizumbukuku ni wewe Nakoma kukusema wewe, jirekebishe chizi wewe. Mtunzi: Abdul-razaq Rajabu Salimu Kutoka: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CHUKIDA) Mawasiliano: 0659392247 abuusalahuddiyn@gmail.com / 5greatlibrary@gmail.com Chungwa tamu ni la Tanga |