MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : U N D U G U - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : U N D U G U - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : U N D U G U (/showthread.php?tid=1941)

SHAIRI : U N D U G U - MwlMaeda - 01-03-2022

U N D U G U
****
1.
Ndugu ni yule mwenzako,
aliye karibu yako,
hata akitoka huko,
kunakoitwa Bamako,
huyo naye nyota yako.
2.
Kama ni Mmarekani,
ni Mwafurika kusini,
asili ye Warabuni,
ama Mwese Ubendeni,
wote wagee thamani.
3.
Maadamu mshirika,
mpo pamoja hakika,
kokote anakotoka,
kwako atahitajika,
mfaane bila shaka.
4.
Anayekukaribia,
maisha mkachangia,
pamwe mkifurahia,
pamoja mkaumia,
huyo ni ndugu sikia.
5.
Nina ndugu siwaoni,
nili’shi nao zamani,
daima wako moyoni,
hawatoki fikarani,
kuwaona natamani.
6.
Ndugu hao walikuwa,
toka pande maridhawa,
za mabara na visiwa,
vema walinielewa,
wakin’jali sawasawa.
7.
Kwao somo nalipata,
la busara nikachota,
kuwa watu wote nyota,
‘sijali wanakotoka,
sote ni ndugu hakika.
8.
Rangi ya ntu ‘siijali,
ukabila usijali,
udini usiujali,
kuwa ni ‘mtu’ ujali,
akubariki Jalali.
****
Rwaka rwa Kagarama,
(Mshairi Mnyarwanda)
Wilaya ya Nyagatare
Jimbo la Mashariki,RWANDA.