SHAIRI : MIOYO YA WANAWAKE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : MIOYO YA WANAWAKE (/showthread.php?tid=1939) |
SHAIRI : MIOYO YA WANAWAKE - MwlMaeda - 01-03-2022 Kalamu ninaandika, Mioyo ya Wanawake, mwenzenu yanishangaza Ina mapenzi lukuki, na huba za kutosheza Kwa hili naipa heko, tena ninaipongeza Mola ameiruzuku. Ukweli usio shaka, Mioyo ya Wanawake, Mungu ilimpendeza Kuipunguzia chuki, na upendo kuongeza Itutoe sononeko, pale linapotokeza Kwenye za taabu siku. Hili ninalianika, Mioyo ya Wanawake, hodari kwa kuuguza Hufanya kile na hiki, uwelewo kuupoza Taabu na masumbuko, yenyewe huyapunguza Na kurejesha shauku. Kusema nalazimika, Mioyo ya Wanawake, tulizo hututuliza Japokuwa zao haki, sisi huzikandamiza Hutupatia vicheko, japo tunaiumiza Kwa mchana na usiku. Tena nina uhakika, Mioyo ya Wanawake, kwa kujali yaongoza Kwenye faraja na dhiki, hutuondoshea kiza Tuibebeni kwa mbeko, tuache kuipuuza Na tuzo tuitunuku. Elenzian_jk(Kalamu Ndogo) elenzianjohns@gmail.com +255625947688| 0655210909 Julai 18, 2019 Dar es salaam-Tanzania |