MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : ASOYAJUWA MATOZI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : ASOYAJUWA MATOZI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : ASOYAJUWA MATOZI (/showthread.php?tid=1936)

SHAIRI : ASOYAJUWA MATOZI - MwlMaeda - 01-03-2022

Nia kuonesha ndiya, sikwamba liwe jelezi,
Ni hiari kupokeya, silifanyi patilizi,
Mazingo yakitukiya, pigaduru kwa walizi,
Usiyejuwa matozi, muole anayeliya.

Si soga nawakupiya, mkaifanya ajizi,
Ama mkamba hekaya, Abunuwasi na ndizi,
Mfuase anoliya, uone yake maozi,
Usiyejuwa matozi, muole anayeliya.

Ziwache zako hisiya, yamwaikaje matozi,
Asadi hakwepi piya, kwayake yalo muhizi,
Utungu ulomwingiya, kumwagika sio kazi,
Usiyejuwa matozi, muole anayeliya.

Nambayo sio ruiya, ukamba ni upuuzi,
Fanya hima nakwambiya, hayano uyamaizi,
Kilio ukisikiya, kaufanye upembuzi,
Usiyejuwa matozi, muole anayeliya.

Kipi chakuajabiya, ukafanya simulizi,
Fazaa ikitukiya, matoni ni mitirizi,
Mhofu mwana kuliya, kuyazuwiya hawezi,
Usiyejuwa matozi, muole anayeliya.

Kwa sita natamatiya, kukwea tena siwezi,
Haya nilo washushiya, si madafu ila nazi,
Usojuwa vumiliya, utapofika ulizi,
Usiyejuwa matozi, muole anayeliya.

MKANYAJI
HAMISI A.S KISSAMVU
0715311590
kissamvujr@gmail.com
kutoka (Baitu shi’ri)
MABIBO * DSM.