SHAIRI : TEZI NA OMO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : TEZI NA OMO (/showthread.php?tid=1931) |
SHAIRI : TEZI NA OMO - MwlMaeda - 01-03-2022 TEZI NA OMO Waume na nisiwani, duniyani tungalimo, Hayano hatuyaoni, tunaifunga midomo, Tumemuwacha Manani, tushenda tezi na omo, Tushenda tezi na omo, naturejee ngamani. Malezi ya kizamani, kichwani tena hayamo, Wanetu ndiyo waneni, kila jambo wao wamo, Ushapotea mzani, tushenda tezi na omo, Tushenda tezi na omo, naturejee ngamani. Mashibu tena sioni, kwa walozidi makamo, Tumekuwa hayawani, ubinadamu haumo, Zimetupotea soni, tushenda tezi na omo, Tushenda tezi na omo, naturejee ngamani. Tu asira wa shetani, kundini mwake tumumo, Kama donda la kichani, hatulioni lilimo, Zimeviza zetu mboni, tushenda tezi na omo, Tushenda tezi na omo, naturejee ngamani. Mvuli kuwekwa ndani, duniya yenda ukomo, Akajivika gauni, ja banati mtazamo, Hatuchukii moyoni, tushenda tezi na omo, Tushenda tezi na omo, naturejee ngamani. Kengele afungwe nani, tuhumu kama hatumo, Tumeingia shimoni, kwakukosa misimamo, Kitanzi kipo shingoni, tushenda tezi na omo, Tushenda tezi na omo, naturejee ngamani. Wakatabahu matini, huchezi bila mfumo, Aliye mkongwe Nyani, amekwepa nyingi fumo, Haitwishi mitihani, tushenda tezi na omo, Tushenda tezi na omo, naturejee nhamani. MKANYAJI HAMISI A.S KISSAMVU 0715311590 kissamvujr@gmail.com kutoka (Baitu shi’ri) |