SHAIRI : NAKUENZI KAMBARAGE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : NAKUENZI KAMBARAGE (/showthread.php?tid=1923) |
SHAIRI : NAKUENZI KAMBARAGE - MwlMaeda - 01-02-2022 SHAIRI : NAKUENZI KAMBARAGE ********** Siwezi kukukumbuka, kimya kimya mtukuka, mwelekezi muafaka, u wa maana hakika, ut’endelea tajika, milele yote milele. **** Kwa dhati toka moyoni, ni shahidi Maanani, Baba ali mhisani, wa wanyonge niamini, alikuwa ni makini, wa haki za binadamu. **** Nyerere wetu shujaa, Afrika aliifaa, wasifa wake wajaa, yote yote mataifaa, mengi mema ulifanzaa, nakuenzi Kambarage. **** Shukurani Maanani, kunigea tungo hini, nikimtaja mwendani, aliyeko mtimani, kulla wa bora imani, amkumbuke Nyerere. *** Rwaka rwa Kagarama, Mshairi Mnyarwanda. |