SHAIRI : LOLIONDO KWA BABU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : LOLIONDO KWA BABU (/showthread.php?tid=1922) |
SHAIRI : LOLIONDO KWA BABU - MwlMaeda - 01-02-2022 Habari natangazia, Kuwapatia uhondo Nchini Tanzania, Kijiji cha Loliondo Watu viguu na njia, Wanoenda kwa vishindo Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Siku imepambazuka, Naamshwa kwa kelele Najifunga yangu shuka, Kutazama walo mbele Tayari washazunguka, Kwa Kasisi Ambakile Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Miujiza imefika, Babu yeye keshaota Wote mloathirika, Anzeni kujikokota Loliondo mkifika, Mizizi inatokota Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Iwapo una nafasi, Usiende mhimbili Ondoa na wasiwasi, Loliondo kuna dili Dawa bei ni rahisi, Kikombe ni buku mbili Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Kashinda madakitari, Walosoma hadi ng’ambo Magonjwa yote hatari, Yalokuwepo kitambo Eti mpaka kisukari, kweli babu ana mambo Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Ukimwi unatutisha, Ugonjwa kama adhabu Waganga wamechemsha, Kutafuta matibabu Kama mbinu zimekwisha, Kajaribuni kwa babu Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Kwa babu kuna vioja, Kabla kutoa tiba Hutangaza yake hoja, Dawa msije kuiba Mnapata mara moja, Sio kunywa mkashiba Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Wala msifanye pupa, Walokwenda ni umati Babu dawa akikupa, Kunywa kwa kombe la bati Usipeleke na chupa, Ukayavunja masharti Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Aponya kila madhara, Hili wengi wanakiri Pengine ni biashara, Katumia muhubiri Kujitoa ufukara, Ajipe na utajiri Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Mara bibi wa tabora, keshaibuka na yake Kujiona ndio bora, Na yeye afaidike Watu kweli ni wakora, Jamani tuwajibike Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Sijui kama ya kweli, Msije mkasusia Mi nahisi utapeli, Mbuzi ndani ya gunia Dawa sijaikubali, Maajabu ya dunia? Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga Namefika kaditama, Dawa zinanitatiza Babu ataniandama, Malenga kuniapiza Ninaogopa lawama, Shairi nimemaliza Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga HAMZA A. MOHAMMED |