ETIMOLOJIA YA NENO 'KANISA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'KANISA (/showthread.php?tid=1918) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'KANISA - MwlMaeda - 01-01-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'KANISA' Neno *Kanisa*[ *Ngeli: li-/ya-, wingi: makanisa]* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Nyumba ya ibada za kikristo, jengo linalitumiwa na watu aghalabu Wakristo kwa ajili ya kumuabudu Mungu. 2. Jumuiya ya kikristo, kundi la waumini aghalabu Wakristo. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *kanisa* (soma: *kaniisatun/kaniisatan/kaniisatin كنيسة)* ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Mahali pa ibada kwa Wakristo (Manaswara). 2. Kundi la waumini Manaswara (Wakristo). 3. Mahali pa ibada kwa Mayahudi. Huitwa pia *biia* *بيعة* . Etimolojia ya neno hili kanisa imekuwa ikigombaniwa baina ya lugha mbalimbali. Wapo wanaodai kuwa etimolojia ya *kanisa* ni neno la lugha ya Kigiriki *εκκλησια* *(eklesia)* lenye maana ya "kukusanya" au "wito". Kuna madai pia kuwa etimolojia ya neno kanisa ni neno la lugha ya Kisiria *ܟܢܫܐ* ( *kansha* ) lenye maana ya "kukusanya" au "umati wa watu". Wapo pia wanaodai kuwa neno kanisa limetokana na neno la lugha ya Kiebrania, " *Kunsi*" ambalo linamaanisha "kusanyiko". Kinachodhihiri ni kuwa neno *kanisa* ( *soma: kaniisatu/kaniisatan/kaniisatin كنيسة*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *kanisa* maana zake katika lugha ya Kiarabu hazikubadilika. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |