SHAIRI: MWAKA MPYA, JIPANGE UPYA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MWAKA MPYA, JIPANGE UPYA (/showthread.php?tid=1912) |
SHAIRI: MWAKA MPYA, JIPANGE UPYA - MwlMaeda - 01-01-2022 MWAKA MPYA, JIPANGE UPYA Mwalimu ametwambia, Lupogo ametamka, Mwaka unapofikia, upya Simama hakika, Kaa ukifikiria, jiandae na zinduka, *Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.* Upya jikazeĀ sikia, jitahidi chakarika, Jua palipo na nia, pambana njia kushika, Kazana na pangilia, malengo utayafika, *Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.* Lima na wako dhuria, tumia zana husika, Lima kilimo huria, cha matunda na nafaka, Lima ukimwagilia, na mbolea ukiweka, *Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.* Tafuta na ulizia, masoko ya uhakika, Chambua na fikiria, amua la muafaka, Sitanie ukalia, usiujaribu mwaka, *Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.* Tingisha na shikilia, jieleze na sikika, Imba wasije kimbia, burudani wanataka, Cheza mpira, kimbia, jiongeze huu mwaka, *Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.* Tama hapa naishia, ya Lupogo kuandika, Kwa ushairi jadiya, masivina sikutaka, Heri ninawatakia, ya shari kuwaepuka, *Mwaka Mpya umefika, upya jipange sikia.* *Khamis S.M. Mataka* *Dar es Salaam, 31.12.2021* |