MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BARAKA' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'BARAKA' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BARAKA' (/showthread.php?tid=1910)

ETIMOLOJIA YA NENO 'BARAKA' - MwlMaeda - 12-31-2021

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BARAKA'

Neno *baraka*[ *Ngeli: i-/zi-]* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: ya:

1. Jumla ya mambo mazuri katika maisha ya mtu.

2. Jina la mtu aghalabu mwanaume lenye maana ya ulinzi na upendeleo wa Mungu kwa mtu katika mambo yote.

3. Mambo yenye kuleta ustawi.

*Kuna methali:* Chambo chema ni baraka ya mvuvi.
*Kuna nahau:* Baraka za Kazole: Baraka nyingi.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *baraka* (soma: *barakatun/barakatan/barakatin بركة)* ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Nafaka maarufu yenye rangi nyeusi inayotumiwa kutibu maradhi, huitwa habbatul Barakah; habbatus Sawdaa (Black Seeds).

2. Ukuaji na kuongezeka (kuwepo ziada).

3. Kheri na ustawi.

4. Tamko: Assalaamu Alaykum wa Rahmatu Llaahi wa Barakaatuhu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *baraka* ( *soma: barakatun/barakatan/barakatin  بركة*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *baraka* maana iliyozingatiwa ni ile ya jumla ya mambo mazuri katika maisha ya mtu na ilibeba dhana ya jina la kipekee la mtu kwa maana iliyotangulia kutajwa. 

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*