MANENO YA KIUTANDAWAZI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: MANENO YA KIUTANDAWAZI (/showthread.php?tid=191) |
MANENO YA KIUTANDAWAZI - MwlMaeda - 06-22-2021 1 2O8 ucku >>>>>Tuonane usiku 2 2takuwa pa1 cku ya j3 >>>>>Tutakuwa pamoja cku ya j3 3 6ki kutu100 lg yko >>>>>Sitaki kutumia lugha yako 4 Nitakwenda PBA x1 >>>>Nitakwenda Pemba mara moja 5 Mm + ww 2tapenda+ x+ >>>>>Mimi na wewe tutapendana sana 6 2kutane x 2 ucku >>>>>Tukutane saa mbili usiku 7 2+kula ma2nda >>>>>Tunakula matunda 8 Bb hajmb kdg>>>>> Bibi hajambo kidogo 9 2me6 xx hv >>>>Tumesita sasa hivi 10 Mm cjui 7bu >>>>Mimi sijui sababu 11 2lia ww >>>>Tulia wewe 12 2+ m2 m1 2 >>>>Tuna mtu mmoja tu 13 Ukifika utanicall >>>>Ukifika utanipigia 14 Cc wte ni wageni >>>>>Sisi wote ni wageni 15 Ni2mie sms >>>>>Nitumie ujumbe 16 Bado dkk kdg >>>>Bado dakika kidogo 17 Km co yy ni ww Kama sio yeye ni wewe 18 Nimeckia ku+ mali ye2 >>>>Nimesikia kuna mali yetu 19 Amelala coz a+umwa Amelala sababu anaumwa 20 Km vp ctokuja >>>>>Kama vipi sitokuja 21 Nitapiga mm cm >>>>>Nitapiga mm simu 22 So umelala >>>>Kwahiyo umelala 23 Cpendi kelele zako bac 2 >>>>Sipendi kelele zako basi tu 24 Kdg ki+mtosha >>>>>Kidogo kinamtosha 25 V2 km iv >>>>Vitu kama hivi 26 Vp bro 2tachat leo? >>>>Vipi kaka tutawasiliana leo? 27 Nipo mku5ni >>>>Nipo mkutanoni 28 Umechukua ha2a gn? >>>>Umechukua hatua gani? 29 Nitakuja j5 chuo >>>>Nitakuja jumatano chuoni 30 2naombwa kuja oficn na rict za malipo j5>>>>Tunaombwa kuja ofisini na risiti za malipo Jumatano 31 Tutakwenda x kwa x >>>>Tutakwenda mara kwa mara 32 2po pmj ktk ili >>>>Tupo pamoja katika hili 33 U+taka k2 gn? >>>>Unataka kitu gani? 34 6ki ki2 >>>>Sitaki kitu 35 Nimefika 4ro >>>>Nimefika forodhani 36 Pa 1 + yote >>>>Pamoja na yote 37 1 kwa 1 >>>Moja kwa moja 38 Wkt huu >>>Wakati huu 39 Ww upo sw >>>Wewe upo sawa 40 Sema mpz >>>Sema mpenzi RE: MANENO YA KIUTANDAWAZI - MwlMlela - 06-26-2021 Kwakweli, baadhi ya vifupisho vya kisasa huwa vinanitatanisha sana |