ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI (/showthread.php?tid=1906) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI - MwlMaeda - 12-31-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFIRITI' Neno *afiriti*[ *Ngeli: a-/wa-]* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: ya: 1. Mtu anayechochea wenzake kufanya maovu. 2. Shetani aletaye madhara kwa watu, maluuni, jini, ibilisi. 3. Mtu mwenye tabia za ujanjaujanja, mdangayifu. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *afiriti* (soma: *ifriit عفريت)* ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Mtu khabithi/habithi, muovu, mdaganyifu. 2. Mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu katika kutenda jambo fulani; mahiri. 3. Jini, shetani, pepo. 4. Kreni inayoinua magari na kadhalika. Kinachodhihiri ni kuwa neno *afiriti* ( *soma: ifriit عفريت*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *afiriti* maana zake zinazohusu jini na mtu mjanjamjanja/mdanganyifu hazikubadilika isipokuwa limeacha maana zingine katika Kiarabu na kuchukua dhana ya mtu anayechochea wenzake kufanya maovu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |