ETIMOLOJIA YA MANENO ' ADHAMA' NA 'ADHANA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO ' ADHAMA' NA 'ADHANA (/showthread.php?tid=1882) |
ETIMOLOJIA YA MANENO ' ADHAMA' NA 'ADHANA - MwlMaeda - 12-28-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' ADHAMA' NA 'ADHANA'. Neno *adhama* [ *Ngeli: i-/zi-]* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. *Nomino*: Hali ya kitu kuwa na ubora. 2. *Nomino:* Mamlaka ya juu kabisa; enzi, ukuu. 3. Heshima kubwa, utukufu katika jambo. 4. Jambo la heshima kubwa. *Mfano* : Kupewa fursa ya kuhutubia Mkutano huu ni adhama kubwa kwangu. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili adhama (soma: adhwamatun/adhwamatan/adhwamatin عظمة ) ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Ukubwa, ukuu. 2. Kiburi, kujiona. 3. Majivuno. Neno adhana [Ngeli: i-/zi-] katika lugha ya Kiswahili ni *nomino* yenye maana ya: mwito unaonadiwa na mwadhini msikitini kwa lengo la kuwaita Waislamu kwenda kufanya ibada. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili adhana (soma: adhaanun/adhaanan/adhaanin أذان ) lina maana zifuatazo: 1. *Nomino*: Tangazo la jambo lolote lile. 2. *Nomino* : Mwito kwa waislamu kwenda kufanya ibada ya Swala. Kinachodhihiri ni kuwa wakati maneno *adhama* (soma: *adhwamatun/adhwamatan/adhwamatin عظمة*) na *adhana* (soma: *adhaanun/adhaanan/adhaanin أذان* ) yalipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa kuwa maneno *adhama* na *adhana* maana zake za msingi katika lugha ya Kiarabu hazikubadilika. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |