MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI: MUHADHARA WA SITA - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI: MUHADHARA WA SITA - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3)
+---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20)
+----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=22)
+----- Thread: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI: MUHADHARA WA SITA (/showthread.php?tid=1846)



FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI: MUHADHARA WA SITA - MwlMaeda - 12-27-2021

MUHADHARA WA SITA
   NYIMBO
Zinaelezwa na baadhi ya wataalamu kuwa ni chochote kinachoimbika. Katika nyimbo tunapata ushairi simulizi na ngomezi.
(a)    Ushairi simulizi
Ni tungo za kinudhumu zinazotungwa kwa kufuata kanuni au kutofuata kanuni za urari wa sauti, mapigo ya sauti na mpangilio wa vipashio vya lugha. Lugha ya kishairi katika fasihi simulizi hupambanuliwa na lugha ya kawaida kwa namna inavyopagiliwa na jinsi inavyoingiliana na muktadha wa utendaji. Kanuni za kishairi hupambanuliwa kwa kufuata wizani (rithimu) maalumu na mawimbi ya sauti,mara nyingi lugha huwa ya mkato, tamathali na mafumbo hutumika.
Ushairi simulizi una tanzu nyingi lakini tunaweza kuzigawa zote katika makundi mawili ambayo ni nyimbo na maghani.
Mgawanyo huu ni kwa ajili ya uchambuzi tu kwani nyimbo nyingi pia ni maghani na maghani mengi ni nyimbo.
Nyimbo – ni kila kinachoimbika; dhanna hii inajumuisha tanzu nyingi baadhi zikiwa za kinathari pia huingia kwenye kundi hili pale zinapoimbwa.
Mambo muhimu yanayotambulisha nyimbo
–   Muziki wa sauti ya mwimbaji au waimbaji
–   Muziki wa ala
–   Matini au maneno yanayoimbwa
–   Hadhira inayoimbiwa
–   Muktadha (mazingira) yanayofungamana na wimbo mf: sherehe, Ibada,tanzia,kazi,n.k
Nui au tanzu kuu za nyimbo za Afrika Mashariki
Mashairi
Kundi hili linaundwa na vipengele mbalimbali kama vile:
(i)         Tumbuizo ; hizi ni nyimbo za kuliwaza au kufurahisha watu kwenye matukio mbalimbali kama msiba, ngoma au haruzi.
Tanzu za tumbuizo
(a)    Bembea/pembejezi; ni nyimbo za kubembeleza watoto na hupatikana katika kila kabila.
(b)    Mbolezi; ni nyimbo za kilio au maombolezo na hutumika kuliwaza wafiwa na kuwaondolea machungu.
©    Nyiso; ni nyimbo za jando au unyago na huimbwa na makabila yenye mila na desturi ya kupeleka watoto unyagoni au jandoni, nyimbo hizi hukusudiwa kuwaasa wari kuhusu majukumu ya kiutu uzima pindi watakapohitimu jando au unyago.
(ii)       Nyimbo za siasa
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa kwenye shughuli za kisiasa kwa lengo la kuelewesha,kuhamasisha,kubeza na kutumbuiza kwenye tukio husika. Mf: ccm… nambari wani, Tumejipanga…….mwaka huu wataisoma, Sasa kumekucha……jogoo limekwishawika Dodomaaa……n.k
(iii)     Tukuzo
Ni nyimbo zinazoimbwa kutukuza au kudhihirisha utukufu na ufahari wa taifa,mtawala,mtu au kitu fulani. Mf: Tazama ramani utaona nchi nzuri…….
Yenye mito na mabonde mengi ya nafakaa…nanenaa kwa kinywa halafu kwa kufikiri nchi iliyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaaa…….majira yetu hayaaaa… yangekuwaje sasa…
Tanzu za tukuzo ni:
(a)    Kongozi; Ni nyimbo za kuaga mwaka au kuadhimisha mwandamo wa mwezi. Nyimbo hizi ni maarufu sana unguja na huchezwa kipindi cha sherehe za kuaga mwaka na huambatana na ngoma ijulikanayo kama Shindwe. Wachezaji huzunguka nyumba hadi nyumba na kupewa chochote wakati wakiimba.
(b)    Nyimbo za dini; Ni nyimbo za kidini ambazo huimbwa na kumtukuza Mungu.
Mfano:
–   Kaswida za kumsifu Mungu
–   Nyimbo za Kikristo kama Tenzi za rohoni, Tumwimbie Mungu na kwaya. Nyimbo za aina hii huwa na maudhui yanayooana na mafunzo ya dini zinazohusika hasa kuhusu Mungu,ibada,dhambi na mapatilizo ya jehanamu na akhera. Nyimbo hizi zinabeba maudhui yanayohusiana na dini zaidi.
©    Nyimbo za taifa; Ni nyimbo za kusifia taifa na huimbwa katika matukio maalumu. Kwa mfano mataifa mengi ya Afrika wimbo wa taifa ni mmoja na asili yake ni wimbo wa Afrika Kusini. (Nkosisikeleeeeliiii Afrikaaa ……. Mumgu ibariki Afrikaaaaa …….Almight God bless Afrikaaaa …….)
(iv)       Chapuzo
Ni nyimbo za kuchekesha na kuhamasisha shughuli au kuwahamasisha watendaji wasichoke wala wasikate tamaa.
Tanzu za chapuzo ni:
Tanzu za chapuzo hugawanywa katika makundi mbalimbali kama vile:
(a)    Kimai; Ni nyimbo zinazoimbwa katika shughuli za uvuvi. Huimbwa ili kuwaondolea wavuvi hofu hasa iwapo ni usiku na vilevile kuwatia ari ya kuvuta makasia.
(b)    Wawe; Ni nyimbo zinazoimbwa wakati wa kazi ya kulima na huimbwa kwa kufuata mapigo ya kupanda na kushuka kwa jembe kadiri walimaji wanavyoinua na kushusha majembe yao kuisakama ardhi.
©    Wimbo wa kutwanga; Wimbo huu huimbwa na wasichana au wanawake wanapopura (kupwaga) ulezi au nafaka yoyote na huimbwa kwa kupokezana wakishindana kupura nafaka. Wimbo huu huleta hamasa na kuwafanya wasichoke mpaka kazi imalizike.
(d)    Nyimbo za vita; nyimbo hizi huimbwa vitani na askari ili kuwahamasisha na kuwaondolea uwoga kwa kuwapandikiza hisia za kizalendo. Mf: ….. Iddi Amini akifa …… mimi siwezi kuliaaa … nitamtupa Kageraaa …… awe chakula cha mambaaa …piga magoti Amini … Amini … piga magoti Aminiiii ….. aaakija toboa … toboa … toboa ….. toboa …  Nyimbo hizi huwasahaulisha kama kuna kufa na hujikuta wakisonga mbele na kumkabili adui.
(e)    Nyimbo za watoto; Nyimbo hizi huimbwa na watoto wakati wa michezo yao,hukusudiwa kunogesha michezo yao. Nyimbo hizi kwa kiasi kikubwa zinasetiri itikadi na falsafa ya jamii kuhusu mahusiano, ndoa na tabia mbalimbali za kibinadamu.
Tenzi au Tendi
Haya ni masimulizi ya kishairi yanayohusu matukio ya kihistoria au kishujaa. Hizi ni nyimbo ndefu za kimasimulizi au kimawaidha ambazo zinahusiana na matukio ya kihistoria, nyimbo hizi zinaitwa tenzi na zinapohusu visa vya mashujaa huitwa tendi.
Mfano: Nyimbo za Issa Matona ni Tenzi, nyimbo za ngoma ya chakacha halikadhalika. Mfano wa tendi ni utendi wa Fumo Liyongo.