MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

Vitanza Ndimi - Printable Version
|
Vitanza Ndimi - Printable Version
+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9)
+--- Thread: Vitanza Ndimi (/showthread.php?tid=184)
|
Vitanza Ndimi - MwlMaeda - 06-21-2021
Vitanza Ndimi
- Sentensi zenye mfuatano wa sauti zinazotatanisha kimatamshi zinapotamkwa kwa haraka.
Mifano
- Wataita wataita Wataita wa Taita.
- Waite wale wana wa liwali wale wali wa liwalii
- Kupa mpe akupao kumpa asokupa si kupa ni kutupa.
- Shirika la Reli la Rwanda
- Hilo lililoliwa ndilo nililolitaka.
- Mchuuzi wa mchuzi hana ujuzi wa mjusi wa juzi.
- Cha mkufuu mwanafuu ha akila hu cha mwanafuu mkufuu hu akila ha
- Pema usijapo pema ukipema si pema tena
- Nguo zisizotakikana zitachomwa zote.
Sifa
- Ni kauli fupi.
- Huwa na mchezo wa maneno.
- Huundwa kwa sauti zinazokaribiana kimatamshi.
- Hutumia maneno yenye maana zaidi ya moja au yenye sauti sawa.
- Hutanza/hutatiza ndimi za wengi wakalemewa kutamka.
- Hukanganya kimatamshi.
Umuhimu
- Kukuza matamshi bora mtu anapoendelea kutamka.
- Kukuza uwezo wa kufikiri haraka ili kujua maana za maneno ili kutamka ipasavyo.
- Kupanua ujuzi wa msamiati.
- Kuburudisha kwa kufurahisha na kuchangamsha.
- Husaidia kutofautisha maana za maneno.
- Kujenga stadi ya kusikiliza.
- Kukuza ubunifu kwa kuteua maneno yanayotatanisha kisauti na kimaana.
- Kujenga uhusiano bora kwa ucheshi.
|