MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
ETIMOLOJIA YA NENO 'UGHAIBUNI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'UGHAIBUNI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'UGHAIBUNI' (/showthread.php?tid=1831)



ETIMOLOJIA YA NENO 'UGHAIBUNI' - MwlMaeda - 12-27-2021

HII NI ETIMOLOJIA YA NENO 'UGHAIBUNI'

Vikita Yusufu: Dkt. Khamisi naomba etimolojia ya neno ughaibuni.
Je, Kenya ni ughaibuni?

ETIMOLOJIA YA NENO 'UGHAIBUNI'
Neno Ughaibuni, linatokana na neno la Kiarabu ( al-)Ghaib ( الغائب) lenye maana ya:
1. -siyokuwepo.
2. - enye kufichikana.
3. -siojulikana.

Waswahili wanalitumia neno hili kuelezea nchi za mbali zisizojulikana (Kwa wakati huo wa zamani)...Amekwenda Ughaibuni.
Ughaibuni ni nchi ya mbali isiyojulikana na msemaji.
Pale nchi hiyo inapojulikana basi hukosa sifa ya kuitwa nchi ya ughaibuni kwani tayari inajulikana.
Nchi ya Kenya haiwezi kuitwa nchi ya ughaibuni kwa kuwa ni nchi jirani; si nchi ya mbali na inajulikana; si ghaibu.

Shukran.

Profesa Kineene Wamutiso:??
Maelezo mazuri Ustadh Mataka. Niongezee, hususa kwa mtazamo wakisufii:  al-Ghaibu/al-Ghaibi-mambo ambayo yajulikana na Mwenyezi Mungu tu, siri habari isiyojulikana  ya akhera, mambo yaliyofichika kwa kiumbe. Masufii wana  Ghaibu'l Huwiyyah (siri ya dhati au ya moyo) na *Ghaibu'l Mutlaq (siri kuu au siri li asirali, siri sirini au siri ya siri - Soma Utenzi wa Siri li Asirali , uliotungwa na Binti Lemba Mwanamwarabu, katika mwaka 1652 B.K.  Utenzi huu wahusu hirizi, ambayo ina majina ya sifa tisini na tisa ( ya Mwenyezi Mungu), ambayo yameficha Siri Kuu. Hirizi hii ilipatikana na kafiri jambazi, muuaji, mbwamtu,  mlaaniwa na mnajisi wake za watu, ambaye aliishi jangwani. Kasiri lake lilikuwa la ajabu sana, hata Shetani Rajimi hakujua lilijengwa kwa siri gani. Kafiri huyu jagina na mfalme wa makafiri aliitwa Anzaruni ( Andharuni katika Kibajuni) na aliwanyanyasa Waislamu akitumia hirizi hii (lakini hakujua siri zilizokuwa ndani yake). Mtume Muhammad akasikia habari zake na akaja na jeshi lake kupigana naye. Vita hivi vilikuwa ni kama zilizala/ mtetemeko wa ardhi. Anzaruni, akiwa ba jeshi kubwa sana kuliko la Waislamu,  aliwashinda mara nyingi lakini Mwenyezi Mungu akamfunulia siri Mtume Muhammad, kupitia kwa malaika Jiburili, na ndege mweusi akampokonya hirizi na kumpelekea jagina wa kivita, Simba Ali. Hata hivyo, Waislamu walishindwa wakiwa na hirizi (Funzo: wasitegemee hirizi kama Anzaruni). Wakaswali hata na baadaye wakamshinda Anzaruni.

Tukirudi kwa dhana hizi
za al- Ghaibu kisufii, masufii huzitumia kueleza hali na sifa za Mwenyezi Mungu. Alimu'l Ghaibi  ni Ajuaye Siri zote, mojawapo ya majina ya sifa ya Mwenyezi Mungu. Angaliaa katika Kaswida ya Hamziyyah, ubeti wa tano:

Dhatil ulumi zilawazo kwa alaimi
Al- Ghaibu'l ndako na masimu ya  Adama

Fasiri sisisi yangu:

Elimu ya dhati itokayo kwa elimu nyingi
Na ile msiyojua ni yako na majina ya Adamu

Fasiri yangu kamili ya ubeti huu:

Wewe pekee ndiwe ulifunzwa zaidi elimu yote ya dunia
Kuliko ye yote yule, hata Adamu ( Adamu alifunzwa robo tu ya elimu ambayo Mtume Muhammad alifunzwa ( tazama Kur'uani Tukufu Surah 2: 28--31)


Maneno: - lawa - toka, zilawazo - zitokazo ( KiNgozi), alalimu - elimu nyingi ( Kiarabu), dhatil ulumi , elimu ya dhati ni yako. Aina za elimu ni kama vile:
: ' Im'ul-Mabad ( elimu ya kawaida au inayohusiana na maneno au sentensi za Kur'uani Tukufu na Hadithi ) na 'Ilm 'ul- Muqasid (elimu kamilifu au inayohusiana na dini, kama inavyoelezwa katika Kur'uani Tukufu na Hadithi. Aidha, kuna ' Ilm 'l-Mukushafa (elimu ya ufunuo au ile ya maarifa ya siri au Nuru iangazayo moyo wa Mwislamu halisi, hata akang'ara kidini na kuwa Sufii kwa kuujua ukweli wa Uislamu. Elimu hii pia hujulikana kama 'Ilm 'l-Haqiqah ( maarifa kuhusu ukweli). Masimu ni majina, masimu ya Adama - Majina aliyopewa Adamu na Mwenyezi Mungu na baadaye (Mwenyezi Mungu) akawauliza malaika kama waliyaelewa majina hayo, kama vile Adamu alivyoyaelewa. Malaika wakamjibu ya kwamba hawakujua zaidi ya yale mwenyewe aliwafundisha.

MAJIBU YANGU:
Naam, hilo lizungumzwalo ni neno ghayb (soma: ghaybun/ghayban/ghaybin غيب ).
Hili ni neno linaloundwa na herufi tatu: Ghayni غ ,  Yaa ي , na Baa ب GHAYBUN غيب na lile lililotangulia kuzungumzwa kabla ni neno GHAIBUN (Soma: ghaaibun/ghaaiban/ghaaibin غائب ) na unaweza kuliarifisha (to make it a definite noun) kwa kuliongezea al (sawa na the katika Kiingereza) na likawa alghaaibu  الغائب .
Neno ghaibu (ghaaibun) linaundwa na herufi Ghayn غ , Alif ا , Hamza ء na Baa ب yaani, GHAAIBUN غائب .

FASILI YA NENO GHAYBU غيب:??
الغَيْبُ : (معجم الوسيط) : (معجم الوسيط)
الغَيْبُ  : خلاف الشهادة.  الغَيْبُ  كلُّ ما غاب عن الاِنساِن، سواء أَكاِن مُحَصَّلاً في القلوب أَم غير مُحَصَّل. يقال: تكلَّمَ عن ظَهْرِ الغَيْبُ  وسَمِعْتُ صوتًا من وراءِ الغَيْبُ  من موضعٍ لا أراه، والجمع غُيُوبٌ.
Tarjama
Kwa mujibu wa Kamusi Muujamu Al-Waswiitwi neno GHAYB ni:
1. -liyojificha; kinyume na kinachoonekana/kinachoshuhudiwa.
2. Kila ambacho kimejificha kwa mwanadamu, kiwe kinachoweza kufikiwa na moyo (kufikirika) au kisichoweza kufikirika. Husemwa: Amezungumza ghayb yaliyofichikana.
Na husemwa pia: Nimesikia sauti kutoka mahali ghayb kusikojilikana; mahali asipopaona.
Wingi wa neno la Kiarabu ghayb غيب ni ghuyuub غيوب na Mola Mlezi ni Allaamu Al-Ghuyuub (soma: Allaamul Ghuyuub, علام الغيوب  Mjuzi mno wa visivyoonekana; vilivyofichika.

غَيب : (معجم الرائد) :
غيب  - جمع،  غيوب  و  غياب  - (اسم)
1- مصدر غاب
2- كل ما غاب عن الاِنساِن : « هو عالم بالغيب »
3- سر
4- شك
5- ما سهل واِنخفض من الأرض.

TARJAMA:
Kwa mujibu wa Kamusi Muujamu Al-Raaid معجم الرائد fasili ya neno ghayb غيب (wingi wake: ghuyuub غيوب na ghiyaab غياب ) ni:
1. Tendo-jina la kitenzi cha Kiarabu ghaab.a غاب (ametoweka/ameghibu/hayupo).
2. Kila kilichojificha kuepukana na binadamu (Mwenyeezi Mungu ni Aalimu Al-Ghayb Mjuzi wa yasiyojulikana).
3. Siri.
4. Shaka.
5. Kilichosahilika na kikainama kutokana (kutokamana) na ardhi.

TAMATI :

Nimetekeleza amri yako Kaka Profesa Daktari Kineene Wamutiso kwa kutayamamu. Basi ukiona upungufu wowote ni ukweli kuwa kutayamamu (kujitwaharisha kwa kutumia mchanga) si kutia udhu (kujitwaharisha kwa kutumia maji).
Asubuhi njema!

Khamis S.M. Mataka