UMUHIMU WA KUTOA ELIMU KWA LUGHA YA KWANZA (KISWAHILI) - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Maendeleo ya Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=11) +--- Thread: UMUHIMU WA KUTOA ELIMU KWA LUGHA YA KWANZA (KISWAHILI) (/showthread.php?tid=183) |
UMUHIMU WA KUTOA ELIMU KWA LUGHA YA KWANZA (KISWAHILI) - MwlMaeda - 06-21-2021 Soma hii, itakusaidia:
Hivi watanzania wanafikiria nini kujifunza maudhui ya Kiswahili kwa kutumia Kiingereza? Ni kama Mchina kuamua kijifunza maudhui ya Kichina kwa kutumia Kiswahili, sio uchizi huo? Au mwingireza kujifunza maudhui yake ya hukooo ulaya kwa kutumia Kichina, si uchizi huo? Na Mswahili wa bongo kutumia Kiingereza kujifunza uraia!!!!!
Nina maswali machache kwenu mnaoamini Kiingereza ni elimu, na si lugha kama zilivyo lugha zingine!
Nchi zote hizo nilizozitaja hapo juu zinatumia lugha zao wenyewe kujielimisha. Lakini nchi hizo zinawazungumzaji wazuri wa Kiingereza kuliko Tanzania.
Ukweli ni kwamba....
Nchi tajwa hapo juu wanajifunza Kiingereza kwa chini ya miaka mitatu nawanakizungumza kwa ufasaha zaidi ya Mtanzania aliyesoma Kiingereza, sekondari hadi chuo kwa miaka zaidi ya kumi!! Umewahi kujiuliza ni kwanini? Kwa ufupi sana nitajaribu kukujibu:
KUNA TOFAUTI KUBWA KATI YA LUGHA YA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZA LUGHA FULANI
Kuna tofauti kubwa kati ya lugha ya kufundishia na kujifunza lugha ya kigeni. Watu wanafikiria kutumia Kiingereza kujifunza vitu kama kilimo cha mbogamboga cha Tanzania ndiyo kujifunza Kiingereza na ndiyo kuelimika. Kumbe Kiingereza kinatakiwa kifundishwe kwa ubora wake, pamoja na mambo yanayohusiana na Kiingereza. Namaanisha ni ujinga kujifunza sheria ya Tanzania ama somo la urai linalohusiana na Tanzania kwa lugha ya Kiingereza wakati kwanza, katiba ya Tanzania imeandikwa kwa Kiswahili, siasa (masuala ya uraia kama vile kampeni) zinafanyika kwa Kiswahili--leo unataka utumie Kiingereza kujifunzia maudhui hayo ya Kiswahili! Kwa nchi zilizoendelea lugha ya kigeni hufunzwa na wazawa (natives) wa lugha hiyo au waliojifunza lugha hiyo kama vile Kiingereza na kuchangamana na wazawa wa lugha, pamoja na kufundisha maudhui yanayohusiana na lugha. Huoni kama ni upungufu wa akili kama leo Mchina atatumia Kiswahili kujifunza nyimbo za Kichina? Huo ndio huohuo upunguani ambao Mchina hakukubali kutumia Kiingereza kujifunza mapishi ya vyakula vya Kichina. Geuza kwa watanzania, ni upunguani kujifunza mambo ya watanzania, na maisha ya waswahili kwa Kiingereza badala ya kutumia Kiswahili! Kumbuka Kiingereza si lugha yetu, ina wenyewe, kubali ukatae, ina wenyewe wanaozungumza kwa ufasaha wake, na Kiingereza vilevile kina utamaduni! Kama vile Kichina kilivyo na utamaduni! Maudhui ya Kiingereza yanajumuisha utamaduni wake. Na hapa kwa vile wanasema tunajifunza Kiingereza cha Uingereza (jambo amabalo pia sikubaliani nalo) lugha ya watu wa Uingereza wana utamaduni wao. Huo ndiyo tungetakiwa kujifunza ili kuweza kuwasiliana na watu hao. Hatuna haja ya kujifunza Kiingereza ili tuweze kuwasiliana sisi kwa sisi, yaani watanzania wenyewe, kwani sisi kwa sisi tunamawasiliano tayari. Mawasiliano yetu yapo kwa lugha ya Kiswahili na lugha zingine za nyumbani kama vile Kichaga, Kipare, Kimasai, Kisukuma n.k Mambo yanayohusiana na lugha ya Kiingereza na ambayo yangeleta maana ya kujifunza Kiingereza, ni vitu kama teknolojia ya watu wa Uingereza, Marekani na sehemu zingine ambazo maudhui yao yanapatikana kwa lugha ya Kiingereza. Mazoezi ambayo wanafunzi wangefanya darasani ambayo yangeleta maana ya kujifunza Kiingereza ni kama vile kutafuta tiketi ya ndege (kwa kawaida zipo kwa lugha ya Kiingereza), katiba ya marekani (ipo kwa Kiingereza), n.k. Hivyo ndivyo wenzetu wanavyojifunza lugha za watu, kikiwemo Kiswahili.
Nakumbusha tena, lengo la kujifunza lugha ya kigeni ni kuweza kuwasiliana na mgeni, siyo kuweza kuwasiliana sisi kwa sisi, sisi tayari tuna lugha na hatuna haja ya kutumia lugha za watu kujielimisha kwa mambo yanayotuhusu. Si akili kuchukua lugha ya mgeni kujielimisha kuhusu mambo yanayotuhusu!!!! Ni kama vile tuseme tutumie lugha ya Kiingereza kuwasiliana hapa JF. Sidhani kama utanielewa sana lakini nitashukuru kama utaelewa kidogo, elimu bora haimaanishi Kiingereza. Elimu bora ni maudhui. Na ili maudhui hayo yawafikie walengwa, ni lazima itolewe kwa lugha inayoeleweka.
Kutumia Kiingereza kunawapa watu majukumu mawili, kujifunza lugha kwanza, halafu kuanza kutafsiri maudhui katika Kiswahili ili kupata ujumbe. Hiyo ni biashara kubwa sana unaipa ubongo, na wachache ndiyo hufanikiwa kufanya biashara hiyo. Wengi wanaishia kukariri na kufaulu mtihani basi. Kuna uwezekano wa kujifunza lugha ya Kiingereza bila kutoa elimu ya Tanzania inayowahusu watanzania kwa kutumia lugha wanasiyoielewa ya Kiingereza. Lugha inayoeleweka ni Kiswahili, itumike kuelimisha watu. Faida za kutumia Kiswahili (kufundishia)
Sasa itakuwaje kwa Kiingereza, lugha ambayo ni muhimu kuijua katika dunia ya sasa?
Kama nilivyotangulia kusema, huna haja ya kupata elimu kwa lugha ya Kiingereza ili kukijua Kiingereza. Wachina wanaojifunza Kiingereza kwa muda mfupi na kukizungumza vizuri zaidi yetu hawajakitumia katika elimu, wamejifunza chenyewe kama chenyewe. Hilo ndilo tunalotakiwa tulifanye.
Hatua zifuatazo zichukuliwe:
Jambo lingine:
Umewahi kujiuliza kwanini wazungu wengi wakizungumza wanasimulia hadithi zao za utoto? Yaani si jambo la kushangaza kumsikia mzungu akisema 'When I was a child....'
Ngoja nikupe siri. Katika elimu kuna kitu kinaitwa 'Connection' (Uunganishaji). Unamfundisha mtoto kuunganisha jambo lolote analojifunza darasani na maisha yake ya kawaida. Kwa mfano, unapomfundisha mtoto sheria ya Newton, na kumtaka aikariri lazima umsaidie kuunganisha sheria hiyo na maisha ya kawaida. Mfano mzuri ni kwamba ni huwa nikiwafundisha wanafunzi wangu wa nje za nchi jambo, huniuliza 'Kwa nini ninatakiwa kujua jambo hili?" Hilo ndilo swali linaloleta 'uunganisho' katika elimu, ama mada, au dhana inayofundishwa. Mwalimu anaposhindwa kujibu swali hilo inaonesha haelewi jambo analolifundisha kwa undani wake. Na si kosa, anaweza kuomba msaada kwa wanafunzi au walimu wenzake. Elimu ya Tanzania haina UUNGANISHO, imeachana kuanzia suala la lugha mpaka maudhui. |