MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
UCHAMBUZI WA DIWANI YA CHUNGU TAMU - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
UCHAMBUZI WA DIWANI YA CHUNGU TAMU - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=78)
+--- Thread: UCHAMBUZI WA DIWANI YA CHUNGU TAMU (/showthread.php?tid=1814)



UCHAMBUZI WA DIWANI YA CHUNGU TAMU - MwlMaeda - 12-25-2021

KITABU: CHUNGU TAMU
MWANDISHI: THEOBALD MVUNGI
WACHAPISHAJI: TPH
MWAKA: 1985
UTANGULIZI
Chungu Tamu ni diwani iliyoandikwa na  Theobald Mvungi  miaka ya 1980. Katika diwani hii mwandishi anaimulika jamii na kuichunguza kwa makini. Anakosoa na kutoa mapendekezo ili wananchi waondokane na machungu yanayowaandama na kuonja utamu ambao utawafikisha kwenye kheri. Katika diwani hii mwandishi ameonesha dhahiri jinsi Uchungu na Utamu vinayotangamana katika harakati zote za maisha ya mwanadamu. Kwa ufupi, tunaweza kusema kuwa diwani hii ni kipaza sauti  kinacholia kwa sauti kali kuujulisha ulimwengu juu ya uchungu unaoiandama jamii yetu ya Tanzania .
MAUDHUI
DHAMIRA KUU;  UJENZI YA JAMII MPYA
Suala la ujenzi wa jamii mpya limezishughulisha fikra  za wanafasihi wengi hapa   Tanzania . Jamii endelevu ni jamii mpya ambayo haina ubaguzi, matabaka, uongozi mbaya, yenye kufuata misingi ya haki na usawa. Jamii iliyojikomboa katika Nyanja zote yaani   kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni  na kifikra. Wanafasihi wa Afrika wanaitaka jamii hiyo ijengwe kwa kufuata misingi ya haki na usawa kwa kila mtu. Wameonesha dhahiri kuwa jamii iliyoachwa na wakoloni ilikua imeoza na hivyo zinahitajika juhudi kubwa ili kuondoa uozo huo.
Nchini Tanzania suala la jamii  endelevu  lilianza mara tu baada ya kupata uhuru na kuimarishwa zaidi wakati wa Azaimio la Arusha. Watanzania walitaka wajenge jamii yenye kufuata misingi ya haki na utu, jamii isiyokuwa na matabaka, jamii yenye viongozi waliotakasika, jamii yenye demokrasia ya kweli, jamii isiyo na unyonyaji wa  aina yoyote ile, jamii ambayo hatamu za uongozi zingekuwa mikononi mwa wakulima na wafanyakazi, jamii isiyo na dhuluma ya aina yoyote, n.k.
Hadi mwandishia anaandika diani hii anaonyesha kuwa  jamii  bado haijafanikiwa kuifikia lengo la kujenga jamii mpya.
Mwandishi ameonesha  vikwazo  mbali mbali vinavyokwamisha ujenzi wa jamii mpya na endelevu hapa nchini na mbinu za kujikwamua kutoka kwenye  vikwazo hivyo.Mwandishi  ametoa mapendekezo ambayo anaamini kuwa endapo jamii itayafuata  itafanikiwa kuijenga jamii  mpya na endelevu. Mbinu hizo ndizo dhamira ndogo ndogo za diwani hii kama ifuatavyo;
  1.  KUPINGA DHULUMA
Dhuluma  ni tendo lisilo la haki, tendo la uonevu, ukatili au uovu. Dhuluma hupingana na haki. Suala la dhuluma hurudisha nyuma maendeleo ya jamii na hivyo ni kikwazo kikubwa cha ujenzi wa jamii endelevu. Suala la dhuluma limemshughulisha sana mwandishi wa diwani hii,katika  shairi la “ Chatu na kuku”  ubeti wa mwisho mwandishi anasema;
Basi  babu akatua akatua,
Funda akajimezea,
Mimi tama imejishikia,
Huzuni imenisaliti,
Kwa chatu kukosa dhati,
Ndipo nikapanga hizi beti,
Ziwe kama ndiyo  hati
Ukumbusho wa huyu dhulumati .
  Katika shiri la “Chatu na Kuku”, mwandishi amelijenga kitaswira kuonesha jinsi wakoloni (chatu) walivyoingia Afrika na kuendeleza dhuluma. Chatu amewakilisha wakoloni na kuku anawakilisha wananchi (Waafrika) walioonyonywa na kudhulumiwa na wakoloni. Mayai ya kuku yanawakilisha mali ghafi waliyodhulumu wakoloni kutoka hapa Afrika.
         Katika shairi la “Chanzo ni Wenye Kauli”, mwandishi anaonesha jinsi ulanguzi unavyosababisha dhuluma katika jamii. Ameonesha kuwa chanzo cha ulanguzi ni upungufu wa bidhaa muhimu, tamaa, pamoja na uzembe toka kwenye vyombo vya dola. Ulanguzi husababisha  rushwa, magendo na hivyo haki haitendeki katika jamii.
Mwandishi anasema;
 “Mianzo tukiijua,
Mipango tujipangia,
Kmwe pasiwe na njia,
Ulanguzi kurudia,
Iwe tu twahadithia,
Mithili historia”.
Katika shairi la “Kademokrasia Katoweka”mwandishi anasema;
       Ya msiba atayetamka,
       Udikteta waja haraka,
        Mtemi na walomzunguka,
        Wawatia raia mashaka,
        Dhuluma yatangazwa fanaka.
 Mwandishi anaonesha jinsi wananchi  wanavyodhulumiwa demokrasia yao ya kutoa maoni yao hadharani. Demokrasia inapokosekana, dhuluma ya kutawala kwa mabavu huendelezwa.
   Katika shairi la “Wengine  Wabaki Taabuni”, mwandishi anajadili juu ya dhuluma wanayoiendesha wakubwa dhidi ya watu wa tabaka la chini. Ameonesha kuwa majambazi wanayo idhini ya kufanya kila jambo kwa wanyonge, kwani hayo majambazi hulindwa na wakubwa. Anaendelea kueleza kuwa dhuluma inayoendeshwa na majambazi  hapa nchini ni njama za walinzi (vyombo vya dola).
Anasema;
“Majabazi wanayo idhini,
Kufanya lijalo akilini,
Na hawataingia nguvuni,
Maana walinzi wamo njamani,
Tabu yaanzia kileleni.”
   Mwandishi anaeleza  kuwa tabu inaanzia kileleni maana yake ni tabu au dhuluma inaanzia kwa wakubwa. Hivyo ili tufanikishe suala  la ujenzi wa jamii mpya ni lazima tujitoe mhanga kupambana na kila aina ya dhuluma katika jamii.
  1. KUFANYA KAZI KWA BIDII
Uzembe na kutowajibika ni kikwazo kikubwa kinachokwamisha maendeleo ya jamii yoyote sile. Jamii yoyote ile yenye viongozi wazembe, viongozi wasiowajibika au wananchi wasiojua wajibu wao daima itabaki nyuma kimaendeleo. Mwandishi anaitaka jamii yetu ijue umuhimu wa kazi na kuwajibika katika suala zima la maendeleo. Mashairi kadhaa katika diwani hii yanasisitiza kuhusu umuhimu wa kufanya kazi ili kuleta maendeleo ya jamii. Mashairi haya ni kama vile “Daktari Askari” (UK 11-24), “Chanzo ni Wenye Kauli” (UK 27-28), “Wimbo Wake Hotubani” (UK 28-29) pamoja na lile la “Wengine Wabaki Taabuni” (UK 32-32).
Katika shairi la “Daktari Askari”, mwandishi anaonesha jinsi waganga wanavyojua umuhimu wa kuwajibika katika kazi yao ya utabibu. Ameonesha kuwa wale waganga waliwahudumia majeruhi kwa bidii wakati wa vita. Hivyo kila mtu anatakiwa kuwajibika kama wale waganga ndipo tutaweza kulisukuma mbele gurudumu letu la ujenzi wa jamii endelevu.
Katika shairi la “Chanzo ni Wenye Kauli” mwandishi anaonesha utekelezaji na uwajibikaji mbovu unavyosababisha rushwa, magendo na ulanguzi katika jamii yetu. Katika shairi hili mwandishi ameonesha dhahiri kuwa uzembe toka kwenye vyombo vya dola ndio umechangia uwajibikaji kuwa mbovu. Anasema;
“Chombo hiki kuzembea,
Chanzo kilichozidia,
Magendo kuyatetea,
Watu kuwasaidia,
Chombo kilididimia.”
Katika shairi la “Wimbo Wake Hotubani” mwandishi anaonesha utekelezaji mbaya wa maazimio unavyochangia kuzorota kwa maendeleo ya jamii yetu. Katika shairi hili, mwandishi ameonesha kuwa viongozi wetu wametuna ofisini na shambani hawingii, wanatumia madaraka vibaya, maagizo ni midomoni bila utekelezaji, kila siku-mchana kutwa wanakunywa na kulewa, n.k. Utekeleaji wao uko kwenye hotuba! Mwandishi anasema;
“Cheo kiko mkononi,
Agizo li mdomoni,
Mchana kutwa ndotoni,
Wimbo wake hotubani,
Raia kazi fanyeni.”
Katika shiri la “Wengine Wabaki Taabuni”, mwandishi anaonesha jinsi uzembe kazini, kutowajibika ipasavyo, usaliti pamoja n rushwa unavyorudisha nyuma utekelezaji mzuri wa maazimio tunayojiwekea. Kwa ujumla mshairi anaitaka  jamii ifahamu na kutambua umuhimu wa kazi na wajibu wa kila mmoja katika jamii ndipo tutaweza kufanikisha kuijenga jamii mpya.
  1. KUWA KIONGOZI MZURI
Suala la uongozi mbaya linaonekana kuwashughulisha sana waandishi wengi wa Afrika. Waandishi wengi wameonesha jinsi ambavyo viongozi wengi walioshika madaraka baada ya mkoloni kuondoka walivyoteka nyara uhuru uliopatikana, kwa hiyo mabadiliko yakawa rangi ya ngozi tu, kwani wananchiwengi waliendelea kuteseka katika umasikini wao.
Nchini Tanzania, pia waandishiwa ushairi kama vile E. Kezilahabi ( Karibu Ndani), T. Mvungi (Raha Karaha na Mashairi ya Cheka Cheka), M.S.Khatibu (Fungateya Uhuru), M.M.Mulokozina K.K.Kahingi (Malenga wa Bara), n.k. wamelijdili suala hili la uongozi kwa mapama sana.
            Mashairi yanayojadili dhana ya uongozi mbaya katika diwani hii ni kama:- “Tishio la Binadamu”, “Chini ya Mti Mkavu”, “Wanajua Kuvumilia”, “Chanzo ni Wenye Kauli”, “Wimbo Wake Hotubani” pamoja na “Shairi la Udongoni”
Katika shairila “Tishio la Binadamu” mwandishi anakemea juu ya uongozi unaotumia mabavu. Mfano mzuri mwandishi anakemea nchi za Urusina Marekani ambazo ni wanachama wenye VETOkwenye umoja wa Mataifa zinavyotumia mabavu kuzikandamiza nchi zisizo na nguvu kisilaha. Mwandish anasema;-
“Kuyasudu mabavu, mwadai tusilotaka,
Maoni yetu chakavu, sawa nguo yamiaka,
Ni pengi penye makovu, nchi zilivyopasuka,
Mabomu yateketeza, waundaji mwafurahi!”
Shairi la “Chini ya Mti Mkavu”mwandishi analaani uongozi unaoendeleza dhuluma katika jamii. Anakemea juu ya uongozi mbaya usiojali maslahi ya wengi, uongozi usiopiga vitaumaskini hapa nchini, n.k.
Shairi la “Wanajua Kuvumilia”, mwndishi analaaniahadi za uongo zinazotolewa na viongozi wetu. Ameonesha kuwa viongozi wetu hawasemi ukweli bali uongo ndio umetawala midomo yao. Sauti ya mshairi inayosikika katika shairi hili lina laani vibaya viongozi ambao hawafiki vijijini kwa wananchi waliowachagua kwa kishindo ili kujionea hali halisi ya maisha wanayoshi. Mwandishi anasema:-
“Afadhali kuimba ukweli,
Wimbo mchomo mkali,
Wimbo, unalilia hali,
Ya vijiji vilivyo mbali,
Kwa wale wasio kauli.”
Katika shairi la “Chanzo ni Wenye Kauli”, mwandishi anajadili juu ya madhara yaletwayo na uongozi mbaya. Ni dhahiri kuwa chanzo cha ulanguzi, rushwa, uzembe, na kila aina ya uovu ni uongozi mbaya.
Shairi la “Wimbo Wake Hotubani” linjadili na kuonesha jinsi ungozi mbaya unavyochangia utekelezaji mbaya wa maazimio na mipango tunayojiwekea.
Katika shairi la “Kademokrasi Katoweka”, mwandishianaonesha jinsi uongozi mbaya unavyozorotesha demokrasia katika bara la Afrka. Demokrasia inapokosekana udikteta, dhuluma, usaliti, rushwa na kukosekana kwa haki hutawala katika jamii.
“Shairi la Udongoni”  lawakumbusha viongozi wajibu waokatika jamii. Mwandishi anasema:-
“Lanikumbusha wajibu,
Kujenga si kuharibu,
Naahidi kujaribu,
Kulinda tulichojenga.”
Hivyo, ili tujenge jamii mpya ni lazima tuwe na uongozi bora. Uongozi mbaya ni kikwazo kikubwa cha ujenziendelevu hapa nchini.
  1. KUWEPO NA DEMOKRASIA YA KWELI
Demokrasia ni mfumo wa kuendesha serikali iliyochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu. Demokrasia inahitajika sehemu yoyote ile ili kuwaruhusu wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru bila wasi wasi au kikwazo chochote. Mashairi yanayoongelea suala la demokrasia ni “M janja yu Mashakani”, (UK 25-26), na lile la “Kademokrasi Katoweka”, (UK 30-31)
Katika shairi la “Mjanja yu Mashakani” mwandishi anajadili juu ya mfumo wa demokrasia ambao umejitokeza miaka ya 1980 kote ulimwenguni. Mfumo huu ni ule wa kupiga sera a chma kimoja na kuingia katika mfumo wa vyama vingi (mageuzi). Katika shairi hili mwandishi anaonesha kuwa mfumo wa vyama vingi umewaamsha wananchi wengi kutoka usingizini na kuanza kutetea haki zao. Hata hivyo, mwandishi anaonesha kuwa wale viongozi waliojilimbikizia madaraka na vyeo mbali mbali wamehofia sana mfumo huu na hivyo hufanya kila mbinu ili kuudididmiza. Viongozi wanaong’ang’ania madaraka ndio wanaohofia mfumo huu. Mwandishi anaonesha jinsi wananchi walivyougomea mfumo wa chama kimoja:-
“Barani migomo baridi, kuugomea mfumo,
Mgomo usokaidi wenye kufumba midomo,
Mfumo uso shahidi , vikao wala misemo,
Ni migomo ya kisiasa, modeli ya kote kote.”
Shairi la “Kademokrasi Kametoweka” linapinga uongozi mbaya barani Afrika.ika shairi hili mwandishi ameonesha kuwa demokrasia inapopokonywa na viongozi wachache, udikteta huota mizizi na kuung’oa huchukua muda mrefu. Hali hii inasababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe katika baadhi ya nchi barani Afrika. Mfano wa nchi hizo ni Jamuhuri ya Watu wa Kongo, Uganda, Burundi, Sierra Leone, n.k. Utawala wa nguvu hurudisha nyuma maendeleo ya bara la Afrika nan chi nyingine za ulimwengu wa tatu ambako hakuna demokrsia ya kweli. Mwandishi anasema:-
“Barani mabavu yatumika,
Dikteta asijeanguka,
Na majungu pia ayapika,
Udikteta pasi shufaka,
Nasimulia ya Afrika.”
Katika shairi mwandishi anaonesha kuwa mabovu yanatumika ili kumlinda dikteta asije akaangushwa kwa kufuata mfumo wa demokrasia ya kweli. Madikteta hao hutumia vyombo vya dola kama vile polisi, jeshi, magereza na mahakama ili kutetea maslahi yao. Kwa ujumla anatoa pendekezo kuwa, ili tuweze kufanikisha kuijenga jaii endelevu hatuna budi kujenga na kudumisha demokrasia ya kweli katika harakati zetu za maisha.
III.              KUPIGA VITA MATABAKA
Katika kushughulikia suala la mgawanyiko wa jamii katika matabaka ya watu kufuatana na madaraka walionayoya uchumi na siasa, msanii ametumia vielelezo halisi kufikisha ujumbe. Mashairi yanayojadili mgawanyiko wa watu kulingana na hali zao ni kama vile “Chatu na Kuku” (UK 2),  “Wengine wabaki Taabuni”,”Thomasi na Doto” (UK 38), “Wimbo wake  Hotubani” (UK 28), pamoja na  lile la “Manzese Mpaka Ostabei” (UK 43).
Shairi la “Chatu na Kuku” limejengwa kitaswira kuonesha tabaka la wadhulumaji (chatu) na tabaka la wadhulumiwa (kuku). Pia shairi la “Wimbowake Hotubani”linadhihirisha mataaka yaliyopo nchini mwetu. Magavana wanawakilisha tabaka la juu (viongozi) na punda na ngamia wamechorwa kitaswira kuwakilisha wananchi wanyonge wanaoteswa na kunyanyasika. Shairi la “Wengi Wabaki Taabuni” linaonesha kuwa, kuna matabaka ya aina mbili katika jamii- tabaka la wachache wanaofurahia maisha na tabaka la wengi wanaoteseka taabuni. Shairi la “Thomas na Doto” linaonyesha jinsi tabaka la wazungu  (watu weupe) wanavyolibagua tabaka la watu weusi (waafrika), hata katika suala la mapenzi na ndoa. Na shairi la “Manzese mpaka Ostabei” linadhihirisha jinsi mgawanyo wa watu katika matabaka unavyoleta tofauti za maisha katika jamii. Watu wa tabaka la juu huishi sehemu za starehe kama vile Ostabei lakini watu wa tabaka la chini (mafakiri) huishi sehemu duni zenye msongamano wa watu kam vile Manzese, jijini Dar es saam.
Kwa ujumla mwandishi ameonesha kuwa mgawanyiko wa watu katika matabaka huleta utengano katika jamii. Ili tuweze kufaulu kuijenga jamii mpya (endelevu) hatuna budi kupiga vita matabaka yaliyoshamiri katika jamii. Lengo liwe kuijenga jamii . Yenye kufuata misingi ya haki na usawa.
  1. KUEPUKA VITA (UHASAMA)
Vita husababisha uhasama katika jamii. Huleta ugomvi na kutokuelewana kwa watu. Vita hurudisha nyuma maendeleo ya jamii. Vita huleta athari mbaya katika jamii. Mfano vifo, umasikini, ughali wa maisha, n.k. Mshairi yanayopingana na suala la vita katika diwani hii ni “Tishio la binadamu” na lile la “Daktari Askari.”
Katika shairi la “Tishio la Binadamu”, mwandishi anaitahadharisha dunia kuwa vita kuu vyanukia. Hii ni kutokana na uhasama uliopo kati ya nchi na nchi pamoja na utengenezaji wa silaha kali kutoka Urusi na Marekani. Kutokana na hali hii dunia nzima sasa iko mashakani juu ya vita. Mwandishi anaendelea kueleza kuwa mashindano ya silahayamekuwa ni mchezo nan chi kubwa zinaona fahari kuzitengeneza.  Anasema:-
“Mashindano ya silaha, yamekuwa ni mchezo,
Wakubwa wanaona raha, kwa silaha waziundazo,
Mabomu yaso na silaha, ndiyo yanawapa uwezo,
Urusi na Marekani, dunia mwaipa adha?”
Katka shairi la “Daktari Askari”, mwandishi anaelezea na kusimulia habari za vita kati ya Tanzania na Uganda mwishoni mwa miaka ya 1970. Katika vita hii, Tanzania ilipata hasara kubwa sana kwani uhalifu, ulanguzi, maendo, rushwa vilishamiri wakati wa vita na baada ya vita. Hivyo katika mashairi haya yote mwandishi anaitaka jamii itakayojengwa iepukane daima na suala la vita.
DHAMIRA NYINGINE
  1. SUALA LA MAPENZI
Mwandishi amejadili aina mbali mbali za mapenzi katika diwani hii. Aina ya kwanza ya mapenzi aliyoyajadili ni yale ya mtu nan chi yake. Haya mapenzi tunayaona katika shairi la “Daktari Askari” ambapo tunona kuwa, wakati wa vita kati ya Uganda na Tanzania raia, wanajeshi, manesi, n.k.walijitolea kwa moyo wa dhati kwenda kupigana ili kuikomboa nchi yao. Mapenzi haya ni ya kweli na dhati. Mapenzi ya Iddi Amina Dada kwa nchi yake hayakuwa ya dhati ndiyo maana alitumia mabavu kuiongoza nchi yake.
Mapenzi mengine kati ya mtu na nchi yake yanapatikana katika shairi la “Ngulu Wapaona” (UK 33-36). Katika shairi hili msanii anaonesha umuhimu wa kuwa na  mapenzi na kwenu (nchi yako) hata kama ni porini. Msaanii anamtaka kila mtu kuthamini kwao ahata kama kuna karaha. Anaonesha kuwa kwenu ni kwenu  na ukuthamini na kukuheshimu kwa raha na Baraka.
Pia kuna mapenzi kati ya mwanamme na mwanamke. Mapenzi haya mwandishi ameyagawa ktika makundi makuu  mawili ya mapenzi ya dhati na yale ya udanganyifu. Mashairi yanayoongelea mapenzi ya dhati ni yale ya “Daktari Askari”, “Thomas na Doto”, “Manzese Mpaka Ostabei” pamoja na lile la “Takumbuka Daima.”  Mashairi yanayoongelea mapenzi ya udanganyifu ni kama vile “Usiwe Mwonja Asali”, “Fikra za Waungwana”.
Mapenzi ya dhati ni  ya kuheshimiana. Mapenzi yasiojali hali au kipato cha mtu. Mapenzi ya uaminifu. Mapenzi kati ya Daktari Adam na Eva katika shairi la “DaktariAskari” yalikua ya dhati, bila kujali kwao au taifa. Hali kadhalika mapenzi kati ya Thomas na Doto yalikua ya dhati bila kujali rangi au taifa. Na mapenzi kati ya Mashaka na Dorothy yalikua ya dhati bila kujali pesa au utajiri. Mapenzi ya dhati husababisha uvumilivu katika maisha. Mapenzi ya dhati huzaa matunda mema katika ndoa, yaani hujenga ndoa za uaminifu. Hivyo mapenzi ya dhati huzaa ndoa za kudumu, ndoa zisizojali rangi, utajiri, utaifa au hali ya mtu. Ndoa za uaminifu zilizotokana na mapenzi ya dhati katika diwani hii ni zile kati ya dakitari Adam na Eva, pamoja na ile ya Mashaka na Dorothy.
Mapenzi ya udanganyifu nayo pia huzaa ndoa za udanganyifu na mara nyingi ndoa hizo huwa hazidumu. Katika shairi la “Usiwe Mwonja Asali”, msanii anaonesha jinsi mapenzi ya udanganyifu yanavyosababish uchumba wa udanganyifu. Pia katika shairi hili msanii anaishauri jamii kuwa ukiwa na mchumba msiwe na tabia za kujamiiana ovyo, bali mpaka mtakapooana. Shairi la “Fikra za Waungwana” linadhihirisha wazi jinsi mapenzi ya udanganyifu yanavyosababisha ndoa za ulaghai. Mwandishi anasema:-
“Mume wangu nakupenda, Joseph amenikuna,
Nimekula naye tunda, ninampenda sana,
Na usifanye inda, mimi ni wako kimwana,
Nitaishi kwa mpango, kwako na kwake Joseph.”
Katika shairi la “Mfereji Maringo” (UK 57), msanii anawashauri wanajamiikuwa wajiheshimukatika suala zima la mapenzi na wawe waaminifu au wasafi na wasiwe Malaya. Kwa ujumla, katika mashairi haya yote, mwandishianaitaka jamii yetu idumishe mapenzi na ndoa za dhati.
  1. NAFASI YA MWANAMKE PAMOJA NA UHURU WAKE KATIKA JAMII.
Mwandishi wa diwani hii amemchora mwanamke katika nafasi mbali mbali. Kwanza amemchora kama mwanamapinduzi na jasiri. Katika shairi la “Daktari Askari” mwanamke ameoneshwa akifanya kazi za kimapinduzi sawa na zile za mwanamme. Mwanamke anpigana vita ili aikomboe nchi yake.
Pili, mwanamke amechorwa kama mtu mwenye mapenzi dhati katika jamii. Katika shairi la “Mapenzi Mpaka Ostabei” linamwonesha Dorothy akiwa na mapenzi ya dhati kwa Mashaka . Hali kadhalika katika shairi la “Daktari Askari linamwonesha Eva akionesha mapenzi ya dhati kwa Daktari Adam.
Tatu, mwanamke amechorwa kama kiumbe laghai, asiye mwaminifu hususani katika suala a mapenzi na ndoa. Haya yote tuayoyaona katika shairi la “Fikra za Waungwana”.
Mwisho, mwanamke amechorwa kama mzazi na ezi katika jamii. Katika shairi la “Manzese mpaka Ostabei”, mwanamke amechorwa kama mzazi na mlezi na hii nafasi inawakilishwa na Dorothy ambaye alimzaa motto na kumlea baada ya kuolewa na Mashaka.
Kuhusu uhuru wa mwanamke, msanii ameleta mjadala juu ya uhuru wa mwanamke, uhuru wa kuolewa na wanaume wawili kama afanyavyo mwanaume kwa kuoa wake wawili au zaidi.
Katika shairi la “Fikra za Waungwana” (UK55-57), msanii anajadili dhamira hii kupitia Anna. Katika shairi hili, Anna ana mume wake (Nania) lakini kwa upande mwingine anampenda Joseph mume wake wa pili. Anna haoni sababu ya kutokuwa na wanaume wawili. Kama asemavyo ubeti wa 11:-
“Mume wangu nakupenda, Joseph amenikuna
Nimekula tunda naye, nampendelea sana,
Ila usifanye inda, mimi ni wako kimwana,
Nitaishi kwa mpango, kwako na kwake Joseph.”
Katika diwani hii, msanii anaonesha kuwa uhuru anaoutaka Anna ni wa kuishi au kuwa na wanaume wawili na huo ndio msimamo wa Anna.
Hata baada ya kesi yake kupelekwa mahakamani, Anna alibaki na msimamo  huo huo. Hali kadhalika majaji walishindwa kutoa hukumu, kwani hakuna sharia inayozui mwanamke kuwa na wanaume wenginkama walivyo wanaume ambao huwa na wanawake wengi.
Lakini swali la kujiuliza ni kuwa, je, mwanamke ana haki ya kuwa na wanaume wawili katika jamii? Hakuna sharia inayomzuia mwanamke kuwa na wanaumewawili lakini mila na desturi ndiyo zinazomzuia mwanamke kuwa na waume wawili. Hivyo ni kutokana na ksoro hizo ndiyo maana anapinga kasoro hizo, kudai uhuru wake wa kuolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja kama mwanaume anavyooa wake wawili au zaidi kwa wakati mmoja. Hivyo anaishauri jamii kuona inaweka wazi sharia zinazohusiana na suala hili. Majaji walishindwa kuhukumu kesi ya Nania- hii ni kwasababu hakuna kifungu cha sharia kinachomzuia mwanamke kuolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja.
III.              UMUHIMU WAKUTOA WOSIA
Msanii katika diwani hii anaishauri jamii kutoa wosia kwa familia zao kabla ya mauti kufika. Katika shairi la “Wosia” (UK58-59), msanii anasema kuwa siku yako ikifika, yaani mauti yanapokufikia ni muhimu kutoa wosia kwa familia yako kuhusu mambo ambayo ungetka wakufanyie.
Msanii anatoa wosia wake kuwa yeye akifa jamii inatakiwa imfanyie mambo yafuatayo:-
Kwisha kuniweka chini,
Udongo kasha funika,
Na nyimbo niimbie,
Katoliki yangu dini,
Halafu nawaambia,
Sheree kafanyeni,
Kawaida ya Tanzia (ubeti 2)
Kwa hali hii anaitadharisha jamii kuwa wosia ni kitu cha muhimu kutoa kabla hujafa n sio wosia wa namna watakavyokufanyia, bali hata kuhusu mali zako na namna ya kumilikiwa baada ya kifo chako.
UJUMBE WA MWANDISHI
  1. Ni lazima tujitoe mhanga ili kutetea wanyonge
  2. Dhuluma, unyonyaji, kutowajibika pamoja na uongozi mbaya ni baadhi ya vikwazo vinavyokwamisha ujenzi wa jamii mpya.
III.              Mshindano ya kutengeneza silaha kwa mataifa makubwa huhatarisha amani uniani.
  1. Demokrasia ya kweli ndiyo njia pekee ya kuendeleza mfumo wa mageuzi hapa nchini na katika nchi nyingine za ulimwengu wa tatu.
  2. Mgawanyiko wa watu katika matabaka husababisha kukosekana kwa umoja na mshikamano katika jamii.
  3. Mapenzi ya dhati yanhitajika katika jamii nan i lazima yadumishwe. Mapenzi ya ulaghai yapigwe vita kwa hali zote.
VII.           Suala la mapenzi na ndoa waachiwe wawili wanaopendana na si maamuzi ya wazazi.
FALSAFA YA MWANDISHI
Mwandishi anaamini itikadi itakavyowatetea wanyonge, yenye kuleta haki na usawa kwa kila mtu. Analaani wizi, dhuluma, udikteta,unyonyaji na kila aina ya uovu. Vile vile anatetea uhuru katika mapenzi na ndoa.
Mwandishi wa diwani hii ana msimamo wa kimapinduzi kwani ameonesha matatizo mali mbali yanazikumba jamii zetu na mbinu za kuondokna na matatizo hyo. Miongoni mwa matatizo hayo ni uongozi mbaya, ulanguzi, dhuluma,rushwa, n.k.
FANI
MUUNDO
Katika ushairi, muundo ni umbo, ploti pamoja na mjengo wa ushairi.Muundo hupatikana kwa kuangalia idadi ya mistari kwa kila ubeti wa shairi linalohusika. Katika diwani hii msanii ametumia miundo changamano. Miundo mikuu iliyotumiwa na mwandishi ni ile ya tarbia (mistari mine kwa kila beti) pamoja na sabilia (mistari mitanona kuendelea kwa kila ubeti).
Mashairi yaliyotumia muundo wa tarbia ni Chungu Tamu” (UK 1), “Tishio la Binadamu” (UK1-2), “Chini ya Mti Mkavu’ (UK 10), “Mjanja yu Mashakani” (UK 25), “Radi ya Kiangazi” (UK32-33), “Shairi la Udongoni”(UK36-37), “Fikra za Waungwana” (UK55-57), “Mfereji wa Maringo” (UK57) pamoja na lile la “Takumbuka Daima” (UK57-58)
Mashairi yaliyotumia muundo wa sabilia ni kama vile:- “Daktari Askari” (UK11-25), “Chanzo ni Wenye Kauli” (UK27-28), “Wimbo Wake Hotubani” (UK28-29), “Wengine Wabaki Taabuni” (UK31-32), “Ngulu Wapaona” (UK33-34), “Chungu na Tamu” (UK34-35), “Usiwe Mwnja Asali” (UK37-38), “Thomas na Doto” (UK38-43), “Manzese Mpaka Ostabei” (UK43-54), pamoja na shairi la “Wosia” (UK58-59). Mashairi mengine yaliyobakia yemetumia muundo wa tarbia kwa baadhi ya beti na nyingine muundo wa sabilia.
MTINDO
Mtindo katika kazi ya fasihi ni mbinu au njia pekee inayotumiwa na waandishi ambayo huweza kumtofautisha mwandishi mmoja na mwandishi mwingine. Katika ushairi, kuna aina mbali mbali za mitindo kama vile mtindo unaofuata kanuni za ushairi wa kimapokeo na mtindo unaofuata kanuni za usasa. Mtindo unaofuata kanuni za ushairi wa kimapokeo hutawaliwa na urari wa vina na mizani, muwala, mara nyingi kuna mfanano kwa kila kituo, huweza kuimbika, n.k. Mtindo unaofuata kanun za ushairi wa kisasa haufuati au haufungwifungwi na kanuni za ushairi wa kimapokeo. Hakuna urari wa vina, mizani, ufanano wa kituo, kuimbika, n.k.
Diwani ya Chungu Tamu ina mashairi yaliyotumia mtindo changamano, yaani mtindo unaofuata kanuni za ushairi wa kimapokeo na ule unaofuata kanuni za  ushairi wa kisasa. Hii ina maana kwamba, mshairi anyakubali mashairi ya in azote mbili (kimapokeo na kisasa).
Vile vile mwandishi ametumia mtindo wa masimulizi kwa baadhi ya mashairi. Katika mashairi ya “Chatu na Kuku”, “Daktari Askri” “Thomas na Doto” na “Manzese Mpaka Ostabei”, Mwandishi metumia mtindo huu ili kufikisha ujumbe kwa jamii aliyokusudia.
MATUMIZI YA LUGHA
Aina ya lugha iliyotumika ni sanifu yenye misemo, nahau na methali, tamathali za semi, mbinu nyingine za kisanaa pamoja na ujenzi wa taswira. Lugha ya kishairi yenye uchaguzi maalum wa maneno (diction) imetumika.
MISEMO, NAHAU NA METHALI
Imetumiwa na mwandishi kwa lengo la kuwasilisha ujumbe kwa jamii husika. Mfano:-
a/ Sasa mwaleta shari (msemo) – uk 7
b/ Umoja ni nguvu (methali) –uk 6
c/ Kuvaa masulupwete (msemo) – uk 48
d/ Ndoa ni fumbo (msemo) – uk 42
e/ Usinawe kwa ulimbo (msemo) – uk 42
f/ Mapenzi hayana mipaka (msemo) – uk 40
g/ Utajichimbia kaburi (msemo) – uk 9
h/ Lakini haikutiwa chumvi mitaani (msemo) – uk 12
TAMATHALI ZA SEMI
TASHIBIHA
i.Maoni yetu chakavu, sawa nguo ya miaka (uk 2)
ii.Macho yao mekundu mithili wvuta bangi (uk 6)
iii.Kwa msikilizaji husisimua mithili filamu za wachunga ng’ombe
iv.Shaba kama maji (uk 12)
v.Kichwa chake kama cha kifutu (uk 38)
vi.Mwili ukamjaa harara kama jinni lililokosa mbuyu (uk 41)
vii.Tumbo lake kubwa kama pipa (uk 50)
viii.Kichwa kidogo kama cha chatu (uk 50)
ix.Mweusi kama kiatu cha jeshi (uk 50)
x.Utaonekana kama kinyago cha kuchonga (uk 12),n.k.
TASHIHISI
– Kifo kimeniita (uk 4)
-Njaa inawasaliti (uk 6)
-Kicheche pia ameapa (uk 7)
-Huzuni imenisaliti (uk 10)
-Katika ile baridi kali, mabomu ya mikono, yakatubusu miguuni (uk 16)
-Vichaka vikawakaribisha (uk 38)
-Taa zawaka kwa maringo (uk 44)
-Jiji lasema hali ngumu (uk 44)
-Mapenzi hayana mpango, yakikanywa zaidi, hayana akili ati (uk53)
-Mioto ikapasuka anga (uk 11), n.k.
SITIARI
=Ushairi ni sukari tamu (uk 1)
=Utoto ni kito (uk 2)
=Yeye alisema dunia ni raha na tabu (uk 2)
=Umaskini ni mzigo (uk 11)
=Wote weusi awa mkaa (uk 45)
TAFSIDA
+Usiwe mwonja asali (uk 37)
+Walipenda faragha (uk 51)
+Dora ana kitu tumboni (uk 54)
+Nimekula naye tunda (uk 56)
TABAINA
-Kuwaza na kuwazua
-Lakini usikubali raha tu, kumbuka na karaha (uk 13)
-Aponya aua  (uk 17)
KEJELI
-Nyie yawafalia, mfanyakazi ya kuchoma na kuuza mkaa (uk 45)
-Wa Manzese atakulisha taka (uk 52)
-Jina lenye ugonjwa wa kaka (uk 52)
-Iweje binti shibe aende kwa omba omba (uk 52)
DHIHAKA
-Ati mchumba, mchumba siye Baraka (uk 52)
MBINU NYINGINE ZA KISASA
TAKRIRI
-Mateka, mateka wapenzi (uk 22), Adamu, machozi (uk 20)
-Je je, je….je nyingi (uk 43), Mateka, Mateka, wapewa (uk 22)
-Mama Dora akaasa akaasa (uk 53)
-Tukanyata, tukanyata tukakaribia Mbarara (uk 16)
MDOKEZO
-Je je je…je nyingi (uk 43)
-Si mganga wa tunguli…(uk 14)
-Sijui yaah yaah…(uk 44)
-Sijui Mashaka…(uk 53)
-Kati yao huyu…!(uk 51)
-Profesa Idd Amin…(uk 19)
-Ikawa nakupenda lakini…
NIDAA
-Ati mie mzee1!
-Ghafla mwewe huyu!
-Umeshituka!
-Mwauzunika nini!
-Kwa hamu ya umoja!
TASHTITI
-Hujisikia wezi wakiomba Mungu kabla ya kwenda huko waendako? (uk 13)
-Wewe mwana –kibarua, hujioni? (uk 49)
MJAZIO
-Yule naam, sio huyo, sijui Mashaka…(uk 53)
-Wawaona wanaopelekewa chai, mikate, karanga, mayai…(uk 13)
-Ndugu mwenyekiti nadhani, labda, pengine, ningependekeza, kwa maoni yangu, kwa mfano tungeliweza….(uk 15)
ONOMATOPEA(TANAKALI SAUTI)
-Lo! (uk 4)
-Loooo! (uk 19)
LUGHA YA KIINGEREZA
-Movement order (uk 14)
-Surrender (uk 17)
-Doctor where College? (uk 18)
-Life President? (uk 19)
-Good Doctor (uk 19)
-My first fiancé (uk 20)
-But this is war sir (uk 20)
-Look Adam. My parents are dead. I am alone (uk 23)
-Sir is that a request or an order? (uk 24)
-Two doctors fighting for no reason (uk 25) n.k.
TAFASIRI  YA MOJA KWA MOJA
=Fomu wani (uk 48)
UJENZI WA TASWIRA
Mwandishi ametumia baadhi ya taswira ili kufikisha ujumbe kwa jamii aliyoiandika. Baadhi ya taswira hizo ni kama vile:-
-Chatu (uk 2)…..Inawakilisha wadhulumaji (wakoloni)
-Kuku (uk2)……Inawakilisha wadhulumiwa (Waafrika)
-Vifaranga (uk 9)….Inawakilisha mali ghafi
-Mjanja (uk 25)….Viongozi wanaoshikilia mfumo wa chama kimoja
-Watwana (uk 25)….Wananchi wanaotaka mabadiliko au uongozi mbovu
-Nuglu (uk 33)….Vijiji, sehemu isiyo na maendeleo, sehemu iliyosahaulika
-Zabibu (uk 42)…..Msichana au mwanamke
MANDHARI
Kitbu hiki kiliandaliwa miaka ya 1980. Na matukio yanayosimuliwa katika kitabu hiki yanazungukia nchi za Afrika ya Mashariki hususani Tanzania na Uganda. Hata hivyo, maudhui ya kitabu hiki yanasadifu huu wa sasa katika nchi yoyote ile ulimwengu wa tatu.
JINA LA KITABU
Jina la diwani hii Chungu Tamu linasadifu yaliyomo ndani ya kitabu. Msanii ameonesha kuwa, baada ya kupita katika machungu na kuamua kupambana nayo ndipo utamu utafuata. Anaitaka jamii itumie kila mbinu kupambana na vikwazo vinavyokwamisha jamii siweze kuupata utamu (ujenzi wa jamii mpya endelevu). Aidha msanii anaonesha kuwa katika maisha, uchungu na utamu havitengamani. Vile vile msanii ameonesha dhahiri kuwa, wananchi wa kawaida ambao ndio wazalishaji wanakula “Chungu” lakini viongozi ambao si wazalishaji wanakula “Tamu”.
KUFAULU KWA MWANDISHI
KIMAUDHUI
  • Ameongelea masuala ambayo yanaisakama jamii yetu katika wakati huu tulio nao. Ameonesha mbinu mbalimbali za kufuata ili kufanikisha suala zima la ujenzi wa jamii mpya.
KIFANI
Amefaulu kutumia miundo changamano, mitindo changamano, lugha ya kishairi pamoja na ujenzi wa taswira.
KUTOFAULU KWA MWANDISHI
  • Lugha imejaa taswira kwa kiasi kikubwa na hivyo msomaji wa kawaida hawezi kuambulia ujumbe wowote. Hivyo amewanyima baadhi ya wasomaji uhondo wa kazi yake.
  • Msanii ametumia lugha ya Kiingereza (kigeni) katika baadhi ya mashairi. Huu ni udhaifu wa mwandishi, kwani anakinyima Kiswahili sanifu nafasi ya kuenea. Vile vile kwa mtu asiyefahamu Kiingereza atashindwa kupata ujumbe.