SHAIRI: MAZAWA YA KILA MWAKA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: SHAIRI: MAZAWA YA KILA MWAKA (/showthread.php?tid=1796) |
SHAIRI: MAZAWA YA KILA MWAKA - MwlMaeda - 12-23-2021 MAZAWA YA KILA MWAKA Mazawa ya kila mwaka, leo azaliwa tena Tarehe imeshafika, Rais mumemuona Khatamu ameishika, na nchi inapambana Tena imesalimika, ipo tuli sasa mbona. Ya Rabbi Mola Karimu, mtoa na kuondoa Nanyanyua kwa Nidhamu, mikono kuomba dua Kwani imenilazimu, leo kwako kukujia, Mpe wetu Muadhamu, kila jema la dunia. Mpe anachokitaka, wepesi umfanyiye Mpe tena kwa haraka, moyoni asiumiye Mpe pasi na mashaka, na siye tufurahiye Mpe mema kwa hakika, nchi aisimamiye. Kheri pasi na mipaka, baraka mmiminiye Neema zipate fika, na maisha yatuliye Na watuwe kuridhika, daima washukuriye Lije hilo kila mwaka, Ya Rabbi muhurumiye. Furaha apate cheka, afya usimnyime Imara kuimarika, mahiri na asimame Na bila kutikatika, mambo yetu yasikwame Naomba kwako Rabbuka, mtu wetu mtazame. Ben Othman Zanzibar Happy birthday Mr president. |