ETIMOLOJIA YA MANENO ' FADHAA' na 'FAZAA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO ' FADHAA' na 'FAZAA' (/showthread.php?tid=1794) |
ETIMOLOJIA YA MANENO ' FADHAA' na 'FAZAA' - MwlMaeda - 12-23-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' FADHAA' na 'FAZAA' Neno *fadhaa* katika lugha ya Kiswahili (kwa mujibu wa Kamusi Kuu ya Kiswahili Sanifu na Kamusi ya Kiswahili ya Karne ya 21) lina maana zifuatazo: 1. *Nomino* : Kosa utulivu wa moyo kutokana na jambo fulani ambalo ama umefanyiwa wewe au umemfanyia mtu mwengine ambalo aghalabu huwa si jema. 2. *Nomino:* Hali ya wasiwasi. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *fadhaa* (soma: *fadhaun/fadha-an/fadhain فذع* ) ni nomino yenye maana ya ' *jeuri* '. Ama neno *fazaa* ambalo ni mashuhuri uswahilini na ambalo linachukuliwa kuwa kisawe cha neno *fadhaa* , katika lugha ya Kiarabu ni nomino inayotokana na kitenzi *faza.a/fazi.a* *فزع* ambacho kina maana zifuatazo: 1. *Faza.a فزع* amefazaika/amefadhaika. 2. *Faza.a ilayhi فزع إليه* ameomba hifadhi/amemba msaada. 3. *Faza.aahu فزعه* amemnusuru/amemsaidia. 4. *Faza.a min nawmihi فزع من نومه* ameamka kutoka usingizini. Hiyo nomino *fazaa فزع* katika lugha ya Kiarabu ina maana zifuatazo: 1. Khofu/hofu na wasiwasi. 2. Kuomba hifadhi/ukimbizi. 3. Kuomba msaada. Kinachodhihiri ni kuwa wataalamu wetu wamelichukua kutoka Kiarabu neno *fadhaa فذع* lenye maana ya ' *ujeuri* ' wakalipa maana ya neno la Kiarabu *fazaa فزع* lenye maana ya khofu/hofu na wasiwasi. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |