MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ABJADI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'ABJADI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ABJADI' (/showthread.php?tid=1778)

ETIMOLOJIA YA NENO 'ABJADI' - MwlMaeda - 12-19-2021

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' ABJADI'

Neno *abjadi* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Seti yenye orodha ya herufi au alama zinazotumika katika mfumo wa maandishi, iliyopangwa katika mpango maalumu na wa kudumu, kila herufi au alama  ikitumika kuwasilisha fonimu moja au zaidi katika lugha  inayonukuliwa.

2.  Seti yoyote ya alama au maumbo, kila moja  ikiwakilisha sauti ya matamshi.

3. Orodha ya herufi za lugha fulani. (Mfano: abjadi za Kiswahili.)

4. Orodha ya herufi za Kiarabu zilizopangwa kwa utaratibu maalumu wa alif, bee, tee, thee; *abtathi* .

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *abjadi* ni moja ya *majina matatu* ya orodha za herufi za Kiarabu kutokana na mpangilio na namna ya kutamkwa kwake. Majina mawili mengine ni: *abtath* na *alfabet* .

Katika lugha ya Kiarabu mpangilio wa herufi zake ni wa aina tatu:
1. *Abjad* :
Huu ni mpangilio wa herufi za Kiarabu ufuatao:
A - B - J - D - H - W - Z - h - TW  - Y - K - L - M - N - S - a - F - SW -  Q - R - SH - T - TH - KH - DH - DHW - dhw - GH.
*اب ج د ه و ز ح ط ي ك ل م ن س ع ف ص ق ر ش ت ث خ ذ ض ظ غ.* 

2. *Abtath* :
Huu ni mpangilio wa herufi za Kiarabu ufuatao:
A - B - T - TH - J - h - KH - D - DH - R - Z - S - SH - SW - DHW - TW - dhw - a - GH - F - Q - K -  L- M - N - W - H - Y.
*ا ب ت ث ج ح خ د ذ ر ز س ش ص ض ط ظ ع غ ف ق ك ل م ن و ه ي* .

3. *Alfabet* :
Huu ni mpangilio uleule wa *abtath* pale herufi zake zinapotamkwa kama ifuatavyo:
Alif - Bee - Tee - Thee - Jiim - haau - Khaau - Daal - Dhaal - Raau - Zaau - Siin - Shiin - Swaad - Dhwaad - dhwaau- ain - Ghain - Faau - Qaaf - Kaaf - Laam - Miim - Nuun - Waaw - Haau - Yaau.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *abjad* *ابجد*  ) na visawe vyake ( *abtath* na *alfabet* yalipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa kuwa *abjadi/abtathi/alfabeti* maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu hazikubadilika. 

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*