MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ADABU' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'ADABU' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ADABU' (/showthread.php?tid=1757)

ETIMOLOJIA YA NENO 'ADABU' - MwlMaeda - 12-17-2021

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ADABU'

Neno *Adabu* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mwenendo mwema wa mtu kwake na kwa watu wengine; tabia nzuri.

2. Kuwa na heshima katika kufanya mambo hasa yanayokubalika na jamii.  (i)Methali: Adabu ni nguo uiachapo hukushusha hadhi yako.
(ii) Msemo: Tua adabu: fanya mtu kuwa na adabu.

3. Malipo anayopewa mtu aliyekosa.

4. Kanuni na taratibu za utumiaji wa kitu au jambo.
(i) Msemo: Adabu za lugha.
(ii) Msemo: Adabu za kazi.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *adabu* ( soma: *adabun/adaban/adabin* *ادب* ) na pia (aadaabun/aadaaban/aadaabin) lina maana zifuatazo:

1. Tabia njema; akhlaki nzuri.

2. Taaluma inayohusika na zao la fikra lililo katika ushairi au nathari. 

3. Ndaki ambayo husomeshwa humo taaluma na maarifa insaniya (mambo yanayohusu ubinadamu na wanadamu.)

4. Kinachozalishwa na akili ya mwanadamu miongoni mwa maarifa.

5. Kazi bora ya sanaa iwe katika ushairi au nathari.

6.  Bahasha.

7. Kwa Waarabu wa zamani elimu ya adabu ILMUL ADAB علم الادب ni elimu iliyokusanya masomo ya: Lugha na *Swarfu* (Sarufi Maumbo), *Usuli wa maneno* , *Nah-wu* (Sarufi Miundo), *Balagha* na Tanzu zake za: *Bayaan* (Rhetoric), *Ma-aan* (Semantic), *Badii-i* (The Art of Metaphors and Stylistics), *Arudhi na Qaafiya* (Kunga za Ushairi), *Hati/Mwandiko* , *Insha* na *Fani ya kuzungumza na umma *fannul Khitwaabah فن الخطابة.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *adabun* *ادب*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *adabu* lilichukua kutoka Kiarabu maana zinazohusiana na tabia njema na ujenzi wa tabia hizo ikiwemo kuadhibu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*