ETIMOLOJIA YA NENO ' FASIHI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO ' FASIHI' (/showthread.php?tid=1756) |
ETIMOLOJIA YA NENO ' FASIHI' - MwlMaeda - 12-17-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' FASIHI' Neno *fasihi* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. *Taaluma* inayohusu tungo za kisanaa za simulizi na andishi kwa mfano hadithi, ngano, methali, misemo, nahau, mashairi, tenzi, riwaya na tamthilia; Fasihi andishi; kazi ya fasihi kwa mfano riwaya na tamthilia katika maandishi; taaluma inayohusu tungo zinazodhihirisha sanaa ya lugha. 2. *(Kivumishi)* : -enye lugha safi na nzuri; -enye usahihi wa kutamkwa, - enye usafi wa maneno, na usahihi wa maana na matumizi. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *fasihi* ( soma: *faswiihun/faswiihan/,faswiihin* *فصيح* ) lina maana zifuatazo: 1. *Kivumishi* : mtu mwenye uwezo wa kuweka wazi tungo za lugha na anayeteua maneno yafaayo kisarufi, kimaana na kijamii na kuyaepuka yaliyo kinyume chake. 2. *Kivumishi* : Maneno fasihi ni maneno yaliyo wazi, na yenye kumvutia msikilizaji na yenye kukubalika akilini. 3. *Kivumishi* : Ulimi fasihi ni ule unaomsaidia mtu kutongoa tungo nzuri na zenye kuvutia. 4. *Nomino*: Maziwa safi yaliyosalia baada ya kuchujwa. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *faswiihun* *فصيح* ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *fasihi* lilichukua kutoka Kiarabu maana Kivumishi (-enye lugha safi na nzuri; -enye usahihi wa kutamkwa, - enye usafi wa maneno, na usahihi wa maana na matumizi.) na likapewa maana mpya ya *taaluma inayohusu tungo zinazodhihirisha sanaa ya lugha,* taaluma ambayo katika lugha ya Kiarabu inajulikana kwa jina la *ADABU/AADAABU (* Soma: *Aadaabun/Aadaaban/Aadaab آداب* (Taaluma inayohusika na zao bora la fikra lililo katika ushairi au nathari.) *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |