ETIMOLOJIA YA MANENO 'HALISI' NA 'UHALIS' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'HALISI' NA 'UHALIS' (/showthread.php?tid=1752) |
ETIMOLOJIA YA MANENO 'HALISI' NA 'UHALIS' - MwlMaeda - 12-16-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'HALISI' NA 'UHALISI' Neno *halisi* katika lugha ya Kiswahili ni kitenzi elekezi chenye maana zifuatazo: 1. Halisi.a, endana, lingana na (bei). 2. Faa. Neno hili *visawe* vyake ni maneno *stahiki*, *pendeza* , *shimiri* na *stahili* . Neno hili linanyambulika na kupatikana neno *halisia* . 3. Neno hili ni Kihisishi chenye maana ya: *kisicho doa wala dosari; kilicho asilia.* 4. Neno hili pia ni kivumishi chenye maana ya: (i) -enyewe ; *rafiki halisi* , rafiki hasa. (ii) - a kweli bila ya uwiano au kufanana na -ingine. 5. Neno hili ni kielezi kwa maana ya: *pasipo mashaka,* *hasa* . Neno *uhalisia* ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Hali ya kuwa bayana, halisi na sahihi. 2. Uhalali asilia wa kisheria. 3. Hali ya jambo, kitu au tendo lilivyo. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *halisi* ( soma: *khaaliswun/khaaliswan/khaaliswini* *خالص* ) lina maana zifuatazo: 1. Kilicho halali. 2. Kilicho safi; kisicho doa. 3. Rangi nyeupe iliyotakata; rangi nyeupe isiyo doa. 4. Kinachomhusu mtu maalumu. 5. Bidhaa isiyodaiwa kodi. 6. Rafiki/mwandani wa kweli. Neno *uhalisi* si neno la Kiarabu bali limesanifiwa kutokana na neno la Kiarabu *halisi* *خالص* . Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *khaaliswun* *خالص* ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *halisi* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika bali Kiswahili kikaongeza maana zingine. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |