MANENO YA KISWAHILI YENYE ASILI YA KIARABU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Maendeleo ya Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=11) +--- Thread: MANENO YA KISWAHILI YENYE ASILI YA KIARABU (/showthread.php?tid=173) |
MANENO YA KISWAHILI YENYE ASILI YA KIARABU - MwlMaeda - 06-21-2021 بسم الله الرحمن الرحيم Kiswahili ni miongoni mwa lugha kuu za Afrika iliyo na wazungumzaji wnaokadiriwa kufikia milioni 100.
Lugha hii adhimu imo kwenye familia ya Lugha za kibantu tawi la Sabaki. Kiswahili ni lugha ya Taifa kwa mataifa manne ya Afrika Mashariki na Kati: Tanzania,Kenya,Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC). Aidha Kiswahili ni Lugha Rasmi katika visiwa vya Komoro pia huchukuliwa kuwa ndio Lingua Franka ya Afrika.
Chimbuko na Asili ya Kiswahili ni mambo yanayobishaniwa na wanaisimu(wataalamu wa lugha) hadi leo.Kati ya hao wanaisimu wapo wanaodai Kiswahili asili yake ni Pijini na Krioli huku wengine wakikazia asili ya Kiswahili kuwa ni Lugha ya vizalia, mbali na wale wanaodai Kiswahili ni Kibantu hali kadhalika wale wanadai Kiswahili ni Kiarabu hasa.
Sababu kuu iliyowasukuma baadhi ya wanaisimu kudai asili ya Kiswahili ni Kiarabu, ni msamiati wa Kiswahili kusheheni maneno mengi yenye asili ya Kiarabu.Japo sikubaliani na wazo hili,nakiri kuwa msamiati wa Kiswahili umeathiriwa mno na maneno ya kiarabu kiasi kwamba mtu hawezi kuzungumza sentensi mbili za kiswahili bila ya kutia ndani maneno yaliyotoholewa kutoka kwenye Kiarabu.
Lengo la Makala hii ni kuwawezesha kubaini baadhi ya maneno muhimu ya Kiswahili yanayotokana na Kiarabu.
Tukianza na neno lenyewe “Kiswahili” latokana na neno la kiarabu سواحلي (Sawāhilī) ambalo huwakilisha dhana ya wingi wa neno ساحل (Sāhil) lenye maana ya (lugha) ya Pwani. Ifuatayo ni mifano ya baadhi ya maneno ya kiswahili yenye asili ya Kiarabu:
KISWAHILI KIARABU/ العربية
Hatari. خطر (khabar) Furahi. فرح (Faraha)
Rafiki. رفيق (rafīq)
Tafadhali. تفضل (tafadhal)
Baridi. بارد(bārid)
Dhamiri. ضمير (dhamīr)
Kamusi. قموس (qamūs)
Huru. حر (hurr)
Habari. خبر (khabar)
Kata. قطع (qata‘)
Msumari. مسمار (musmār)
Kitabu. كتاب (kitāb)
Mahali. محل (mahal)
NYAKATI MBALIMBALI
Hapa Kiarabu kimeathiri mno Kiswahili.Majina ya nyakati yamechukuliwa hasa kutokana na majina ya Swala tano za Kiislamu: KISWAHILI. KIARABU/العربية
Asubuhi. صبح (subh)
Dakika. دقيقة (daqīqah)
Saa. ساعة (sā‘ah)
Wakati. وقت (waqt)
Alasiri. العصر (al-‘asr)
Magharibi المغرب (al-maghrib)
Alfajiri. الفجر (al-fajr)
Karne قرن (qarn)
Siku saba za wiki kwa Kiswahili huanza na neno “Juma” lililotokana na neno la Kiarabu جمعة . Majina mawili tu ya siku za wiki hata hivyo ndiyo yanatokana na Kiarabu:
KISWAHILI KIARABU/العربية
Alhamisi الخميس (al-khamīs) Ijumaa الجمعة (al-jumu‘a)
MAJINA YA WANYAMA
Majina ya wanyama katika lugha ya Kiswahili karibu yote yana asili ya Kibantu isipokuwa machache sana yana asili ya Kiarabu: KISWAHILI. KIARABU/العربية
Tausi. طاوس (tāwūs) MAJINA YA NAMBA
Kiarabu kimechukua nafasi kubwa katika mfumo wa Kuhesabu wa lugha ya Kiswahili mfano: KISWAHILI. KIARABU/العربية
Nusu. نصف(nisf)
Robo. ربع (rubu‘)
Sita. ستة(sittah)
Saba. سبعة(sab‘ah)
Tisa. تسعة (tis’ah)
Ishirini عشرين(‘ishrīn)
Thelathini. ثلاثين(thalāthīn)
Arobaini. أربعين(arba‘īn)
Hamsini. خمسين(khamsīn)
Sitini. ستين(sittīn)
Sabini. سبعين(sab‘īn)
Themanini. ثمانين(thamānīn)
Tisini. تسعين(tis’īn)
Mia. مئة(mi’ah)
Elfu. ألف(alf)
DINI
Msamiati mwingi utumikao katika dini ya Kiislamu na Kikristo una asili ya Kiarabu: KISWAHILI. KIARABU
Ibada عبادة(‘ibādah) Msikiti. مسجد(masjid)
Kanisa. كنيسة(kanīsah)
Zaka. زكاة(zakāh)
Sadaka. صدقة(sadaqah)
Malaika. ملائك(malāikah)
Shetani. شيطان(shaitān)
Thawabu. ثواب(thawāb)
Dhambi. ذنب(dhanb)
Kasisi. قسيس(qasīs)
Imamu. إمام(imām)
Kitubio. توبة(thawāb)
Ingawa hii ni mifano michache tu ya maneno ya Kiswahili yenye asili ya Kiarabu hata hivyo inatoa taswira nzima ya taathira ya Kiarabu kwenye Kiswahili.
Hadi wakati mwingine wenu mdau wa Kiswahili:
Mwl A.Raphael
Liwale-Lindi
2019
|