SHAIRI: TIYANI-FATIHA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: TIYANI-FATIHA (/showthread.php?tid=1704) |
SHAIRI: TIYANI-FATIHA - MwlMaeda - 12-11-2021 TIYANI-FATIHA ya mwenda omo na tezi, hachi kurudia ngama, Nakuja kwako mwenyezi, mie mtu si mnyama, Ningalikuwa ni ndezi, niwe na mkia nyuma, singalilia machozi, nikakumbuka ya nyuma, Umenipa mang'amuzi, yangu mambo kuyapima, Nimepima siku hizi, mizani inapindama, Maasia nimehozi, haki yamezidi kima, Ewe Bwana mtetezi, ndiwe mgawa uzima, Nitapokoma pumuzi, tafadhali niwe mwema. Niwe mwema Ee Rahimu, unayetoa Rehema, Nakuomba nirehemu, nitakasike mtima, Mithili mwendawazimu, asotiwa mahakama, Wala usinihukumu, motoni ukanichoma, Ahera ni yangu hamu, palipo mahali pema, Niondolee haramu, penye kosa tia vema, Umri wangu makamu, dhambi zimejaa pima, Maombini ninadumu, shetani hunisakama, Subuhanna wa Karimu, nokoe mimi kilema. Kilema sio wa macho, ja kiwete mchutama, La hasha kitu kilicho, roho yangu si salama, Hizi dhambi kochokocho, tatizo zaniandama, Wangu mwili utakacho, ndicho kiupacho tama, si kile ukitakacho, roho ipatapo homa, maana nikuombacho, nipe roho ilo njema, najua kwa kiwakacho, dumu huisha kuzima, Kwako nikililiacho, unipe yako huruma, kiumbe ukipendacho, mwisho nibaki salama. Mwisho wa mtu kunuka, najua zama na zama, Mana nafanya haraka, wenda leo ndo kiama, nikifa ni takataka, yatoka yangu heshima, hapo roho itatoka, yendapi siwezi sema, kiwa kwako itafika, nikawa tena mzima, sinandikie waraka, kunangushia lawama, bali nondoe mashaka, niache kushika tama, niwe nao malaika, niimbe nao selema, huku kule kuzunguka, tukuimbie Rahima. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |