MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA SABA : UNYAMBULISHAJI KATIKA KISWAHILI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=22) +----- Thread: MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA SABA : UNYAMBULISHAJI KATIKA KISWAHILI (/showthread.php?tid=1626) |
MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA SABA : UNYAMBULISHAJI KATIKA KISWAHILI - MwlMaeda - 12-01-2021 MUHADHARA WA SABA
UNYAMBULISHAJI KATIKA KISWAHILI
Unyambulishaji ni dhanna inayohusu upachikaji wa mofimu katika mzizi wa neno.
Mfano ;
(a) a-na-lim-a
(b) ki-lim-o
© u-lim-a-ji
(d) wa-na-lim-ian-a
Ukichunguza mifano hiyo ya upachikaji wa mofimu utabaini kuwa mofimu zilizopachikwa zinaathiri maana ya mzizi pamoja na mfuatano wa maneno hayo katika sentensi.
Mfano:
(a) Juma analima mashamba mengi
(b) Kilimo kinafundishwa shuleni
© Ulimaji wa pamba ni mgumu
(d) Juma ni mkulima hodari
(e) Juma na ali wanalimiana shamba
Kutokana na mifano hiyo unyambulishaji unaweza kuwekwa katika makundi mawili ambayo ni uambishaji na mnyambuliko.
Mfano
* Uambishaji
Uambishaji ni upachikaji wa viambishi katika mzizi wa neno pasipo kubadili kategoria ya neno.
Katika kiswahili uambishaji hutokea zaidi kabla ya mzizi wa neno. Hii imefanya watu wengi kufikiri kuwa uambbishaji ni kupachika tu viambishi kabla ya mzizi.Mofimu za uambishaji huitwa pia viambishi ambatishi. Viambishi ambatishi hufanya kazi mbalimbali za kisarufi kama kudokeza nafsi, ngeli, njeo, urejeshi, yambwa, yambiwa, n.k
Mfano:
UAMBISHAJI KATIKA MANENO YA KATEGORIA NYINGINE
Uambishaji hutokea pia katika maneno ya kategoria nyingine zaidi ya vitenzi.
(i) Uambishaji wa nomino.
Nomino zinazopokea mofimu ambatishi ni zile zenye umoja na wingi.
Mfano:
Umoja Wingi
M-toto Wa-toto
M- tume Mi-tume
Ki-ongozi Vi-ongoz
Mu-enzi Wa-enzi
(ii) Uambishaji wa vivumishi
mfano
umoja wingi
m-dogo wa-dogo
ki-chafu vi-chafu
ki-baya vi-baya
m-refu wa-refu
NB:Uambishaji sio miongoni mwa njia za uundaji wa maneno mapya kwa sababu maneno hayabadili kategoria.
* Mnyambuliko ni upachikaji wa viambishi katika mzizi wa neno vinavyobadili kategoria ya neno.
Mfano
Cheza
Mchezaji
Mchezo
Tuliocheza
Wametuchezea
Viambishi vya mnyambuliko huitwa viambishi nyambulishi na neno jipya kutokana na unyambuaji huitwa (kinyambuo) – ( vinyambuo).
NB: Unyambuaji ni mojawapo ya njia za uundaji wa maneno mapya
kwa sababu njia hii inahusu mabadiliko ya kategori ya neno.
|