MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA TANO: DHANNA YA MZIZI NA SHINA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=22) +----- Thread: MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA TANO: DHANNA YA MZIZI NA SHINA (/showthread.php?tid=1625) |
MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA TANO: DHANNA YA MZIZI NA SHINA - MwlMaeda - 12-01-2021 MUHADHARA WA TANO: DHANNA YA MZIZI NA SHINA MAANA YA MZIZI Mzizi/kiini cha neno ni ile sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondolewa viambishi awali na tamati. Au Mzizi ni sehemu ya neno isiyobadilika baada ya neno kufanyiwa mnyambuliko. Mzizi huweza kujitokeza katika aina mbalimbali za maneno kama vile vitenzi, nomino, vivumishi, viwakilishi, n.k (i) Mzizi katika vitenzi Mfano: – Juma anasoma kitabu – Baba analima shamba ii) Mzizi katika nomino mfano: – kusoma kwake tunakupenda – mtoto anacheza – watoto wanacheza – kijana analima – vijana wanalima iii) Mzizi katika vivumishi Mfano – mwema-wema – bovu-mabovu – mdogo-wadogo iv) Mzizi katika viwakilishi mfano – Ambaye anaumwa aje – Ambalo umenunua halifai – Ambacho umesema kinakera – mimi-miye – sisi-siye – wewe-weye – nyinyi-nyiye DHIMA YA MZIZI Mzizi hutumika kuunda maneno mapya kwa kutumia viambishi. Mfano
Utambuzi wa mzizi katika neno huweza kufanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile: 1. Njia ya mnyambuliko Ili kupata mzizi wa neno kwa njia hii sharti neno linyambuliwe kwanza. Neno likishanyambuliwa sehemu isiyobadilika huwa ndiyo mzizi. Mfano Soma Somesha Somewa Tulimsomesha Msomi 2. Mbinu ya umoja na wingi Njia hii hufaa zaidi kwa maneno yenye asili ya nomino, vivumishi na viwakilishi Mfano Umoja wingi Mtoto watoto θJembe majembe Kijana vijana Mdogo wadogo 3. Njia ya umbo la ndani Hapa neno hupaswa kurudishwa katika umbo lake la ndani. Kama ni kitenzi kikiishia na irabu “a” basi hiyo irabu “a” ikiondolewa kinachobaki ndiyo mzizi. Iwapo kitenzi kina asili ya kigeni kitaishia na irabu tofauti na “a” na hilo neno zima huweza kuwa ndio mzizi/shina. Mfano Neno Muundo ndani Mzizi Walisomeshwa soma -som- Walipikishwa pika -pik- Tutamsalia Sali -Sali- Mnastarehesha starehe starehe Shukuru shukuru shukur- MAANA YA SHINA Shina la neno ni mzizi wowote wa neno uliofungiliwa kiambishi tamati maana. Mfano Mzizi Shina Pig+a – piga Som+a – soma imb+a — imba SHINA = MZIZI+a
MZIZI = SHINA-a
Uhusiano wa mzizi na mofimu nyingine katika maneno Mzizi huwa na viambishi ambavyo hupachikwa mwanzoni na /au mwishoni mwa mzizi wa neno. ===> Viambishi awali V.A) hufanya kazi kama vile kudokeza nafsi, njeo, urejeshi, yambwa, yambiwa n.k ===> Viambishi tamati (V.T) hufanya kazi ya kudokeza kauli mbalimbali za matendo. |