ETIMOLOJIA YA NENO ' MUTRIBU' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO ' MUTRIBU' (/showthread.php?tid=1624) |
ETIMOLOJIA YA NENO ' MUTRIBU' - MwlMaeda - 12-01-2021 ETIMOLOJIA YA NENO ' MUTRIBU'. Mutribu (wingi: watribu), katika Lugha ya Kiswahili) ni neno (nomino) lenye maana: 1. mwanamuziki katika bendi ya taarab, anayeimba katika kikundi cha taarab. 2. mpiga vyombo au mwimbaji katika bendi ya muziki wa taarab. Neno hili (mutrib) asili yake ni Kiarabu na huko ni 'mutw-ribun/mutw-riban/mutw-ribin مطرب' neno litokanalo na kitenzi cha Kiarabu atw-raba اطرب (amemfanya asisimke, ayumbeyumbe na afurahi kutokana na sauti yake nzuri./amemfurahisha). Katika Lugha ya Kiarabu neno (mutw-ribu) lina maana zifuatazo: 1. Mwimbaji mwenye sauti nzuri anayekonga nyoyo za wasikilizaji. 2. Njia/barabara nyembamba. 3. Anayewafanya watu wasisimke, wayumbeyumbe na wafurahi kutokana na sauti yake nzuri. Neno hili 'mutribu' lilipoingia katika Lugha ya Kiswahili limejifunga na muziki wa taarabu na likajumuisha mwanamuziki mpiga vyombo wakati kiasili katika Lugha ya Kiarabu linamuenea mwimbaji yeyote mwenye sauti nzuri. Shukran sana. Na; Khamis Mataka |