MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA NNE: KUTENGANISHA MOFIMU NA ALOMOFU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=22) +----- Thread: MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA NNE: KUTENGANISHA MOFIMU NA ALOMOFU (/showthread.php?tid=1623) |
MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA NNE: KUTENGANISHA MOFIMU NA ALOMOFU - MwlMaeda - 12-01-2021 MUHADHARA WA NNE: KUTENGANISHA MOFIMU NA ALOMOFU
Lugha ya Kiswahili ni lugha ambishi hivyo ina maneno ambayo huundwa kwa mwandamo wa kisafu wa mofimu. Mofimu hizi hupachikwa kabla na baada ya mzizi kwa mfuatano ulio bayana.
Mfano;
A B
(a) anasoma a-na- som-a
(b) apikiwe a-pik-iw-e
© fungana fung-an a
Utenganishaji wa mofimu katika maneno hayo unaonekana ni rahisi kwa kuwa miundo ya maneno hayo inafahamika.
Tunapotenganisha mofimu za lugha tusiyoijua ni lazima tuwe na miundo yenye ruwaza zinazolingana ili tuweze kufananisha maana na maumbo mapya yanayoandamana na maana mapya.
Mfano;
(a) alatambuka – atatembea
(b) mulatambuka – mtatembea
© balatambuka – watatembea
(d) mukatambuka – mlitembea
(e) balayajula – watatambaa
Ingawa lugha hii yawezekana hatuitambui bado tunaweza kutenga mofimu zake kwa urahisi kwa kuwa kuna ruwaza zinazofanana na zile za lugha tunayoifahamu. Kutokana na data ya lugha ya hapo juu (kihaya)kuna mofimu zifuatazo.
Mofimu za za:
//nafsi//——— (a) -3-umoja
——– (mu) -2-wingi
—— (ba) -3-wingi
//njeo//———– (la) -ijayo
———– (ka) -iliyopita
//mzizi//———- tambuk –
———– yajul –
KANUNI ZA KUTENGANISHA MOFIMU
(a) kanuni ya kwanza; zingatia maumbo yenye maana sawa. Maumbo hayo huweza kufanana au kuhitilafiana kiumbo lakini hutokea katika mazingira yaleyale.
Mfano;
Mofimu
——— (u)-2-umoja
———- (m)-2-wingi
———- (tu)-1-wingi
————- (li)-iliyopita
————– (na)-iliyopo
——— (m)-yeye
———- (ni)-mimi
———– (ji)-binafsi
(b) kanuni ya pili; Hapa kinachozingatiwa ni maumbo yenye maana moja lakini yasiyo na umbo sawa la kimofolojia.
Mfano;
b )mvulana wavulana
mofimu
mofimu za idadi
//umoja//———m/-k
——– mw/-i
//wingi//——— wa/-k
———- w/-I
© Kanuni ya tatu; Kanuni hii inadai kuwa alomofu moja au zaidi zimo katika mtawanyo mkamilishano ambapo moja ikitokea basi ya pili haitokei. Yambwa na yambiwa haziwezi kutokea katika mazingira yale yale.
Mfano
Baba alinimpigia mimi simu
Sisi tuliwamuona nyinyi
Yeye alimwakuta wao
– (m) na (mu)
– (wa) na (w)
Zimo katika mtawanyo mkamilishano au mgawanyo wa kiutowano
(d) Kanuni ya nne; Umbo moja na zaidi huweza kuwa katika mpishano huru kama maumbo hayo yana maana moja na yametokea katika mazingira yaleyale.
Mfano
ngombe badala ya ng’ombe
khabari badala ya habari
lafiki badala ya Rafiki
ntoto badala ya mtoto
(e) Kanuni ya tano; inadai kuwa maumbo yenye maana tofauti ni
mofimu na maumbo tofauti yenye maana sawa ni alomofu.
MATATIZO YA KUTENGANISHA MOFIMU
Mfano:
(i) θ+chungwa : ma+chungwa
(j) θ+bega : ma+bega
(k) θ+jiwe : ma+we
(l) θ+shati : ma+shati
Katika mifano hiyo mofimu za umoja ni //θ// na za wingi ni //ma//
Mfano:
(i) Fupi – fupika –fupisha
(ii) Refu – refuka –refusha
(iii) Kau – kauka – kausha
Mifano hiyo ina maneno asilia na maneno unde. Maneno (fupi na refu) ni maneno asilia ya maneno unde fupisha na refusha. Lakini (kau) sio neno asili la neno (kauka na kausha) kwa sababu neno hilo (kau) halikubaliki kwa maneno ya namna hiyo.
Mfano:
Mwanajeshi
Mu-ana-jeshi
Mw-ana-jeshi
Mw-an-a-jeshi
Mw-anajeshi
Maneno mwambatano yanaundwa kwa mzizi zaidi ya mmoja hivyo huwa ni vigumu kubaini mofimu ni zipi na mizizi ni ipi.
|