ETIMOLOJIA YA NENO "SHAGHALABAGHALA" - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "SHAGHALABAGHALA" (/showthread.php?tid=1618) |
ETIMOLOJIA YA NENO "SHAGHALABAGHALA" - MwlMaeda - 11-30-2021 ETIMOLOJIA YA NENO ' SHAGHALABAGHALA'. Shaghalabaghala katika Lugha ya Kiswahili) ni neno (kielezi), lenye maana ya: hovyohovyo/ovyoovyo, bila utaratibu unaoeleweka, hobelahobela. Neno hili (shaghalabaghala) asili yake ni Kiarabu na huko ni Sentensi yenye maneno mawili: la kwanza, kitenzi cha Kiarabu shaghala شغل ameshughulika/amefanya kazi na la pili jina/nomino baghlu بغل (mnyama aliyezaliwa na mama farasi na baba punda). Sifa ya mnyama huyu ni kuwa mvumilivu kama punda na anamiliki mwendo kasi kama farasi. Waalimu wetu madrasa wakati wakitafsiri Kisa cha Miraji (Safari ,ya kimiujiza ya Mtume Muhammad - Allaah Amrehemu na Ampe Amani - kutoka Makkah hadi Baitul Maqdis, Jerusalem, kwa kutumia sehemu tu ya usiku mmoja) walitafsiri baghlu بغل kuwa ni nyumbu. Lakini kwa mujibu wa sifa za baghlu aliye mnyama chotara wa farasi na punda ni kuwa mnyama huyu ni tasa, hazai. Hivyo neno la Kiswahili shaghalabaghala kiasili lina maana ya 'kazi ya mnyama baghlu (chotara wa punda na farasi) kazi ambayo ni hobelahobela. Shukran sana. Na; Khamis Mataka |