MCHANGO WA SARUFI GEUZI ZALISHI KATIKA UCHAMBUZI WA LUGHA YA KISWAHILI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: MCHANGO WA SARUFI GEUZI ZALISHI KATIKA UCHAMBUZI WA LUGHA YA KISWAHILI (/showthread.php?tid=1615) |
MCHANGO WA SARUFI GEUZI ZALISHI KATIKA UCHAMBUZI WA LUGHA YA KISWAHILI - MwlMaeda - 11-28-2021 MCHANGO WA SARUFI GEUZI ZALISHI KATIKA UCHAMBUZI WA LUGHA YA KISWAHILI
Katika kuanza kuangalia mchanngo wa sarufi geuzi zalishi , tutaangalia maana ya sarufi geuzi , sarufi zalishi na sarufi geuzi zalishi kwa ujumla
Sarufi geuzi kwa mujibu wa Matinde (2012) anasema sarufi geuzi ni utaratibu wa kubadili maumbo ya maneno kuwa maumbo mengine kwa kufuata kanuni maalumu.Sarufi hii hujengwe kwa wazo kwamba katika lugha kuna sentensin ambazo huwa ni za msingi, ambazo kutokana na kaida mahsusi sentensi zingine huweza kuzalishwa kutokana na sentensi hizo.Ugeuzi huathiri muundo wa sentensi na wala si maana ya sentensi.Kwamba, hata baada ya ugeuzaji maana ya sentensi ya kwanza haibadiliki Kwa mfano
(a) Rugatiri amemchapa Mugyabuso
(b) Mugyabuso amechapwa na Rugatiri
Katika sentensi hizi tunaona kuwa sentensi ya kwanza imegeuzwa umbo na kuwa sentensi ya pili yaani;
Ugeuzaji hutekeleza mambo yafuatayo;
(a)Uchopekaji wa viambajengo
(b)Upanguaji wa viambajengo
©Udondoshaji viambajengo
(d)Uunganishaji wa tungo
Sarufi zalishi
Sarufi hii hueleza namna ambavyo lugha inavyotumiwa na watumiaji wake hususani jinsi wanavyotumia kanuni chache katika lugha yao kuzalisha sentensi nyingi na zisizo na kikomo.Hivyo kutokana na uwezo huu mzawa wa lugha huweza kuunda tungo ambazo ni sahihi na zile ambazo si sahihi.Sarufi zalishi ina dhana zifuatazo
(i) Umilisi
(ii)Utendaji
(iii)Umbo anila nd
(iv)Umbo la nje
(v)Uchamko
Sarufi geuzi zalishi inahusishwa na mawazo ya Noam Chomsky katika kitabu chake kiitwacho Syntactic Structures (1957).Katika kitabu hivi mwanaisimu huyu alizua dhana ya sarufi zalishi ambayo ilidhirisha mapinduzi ya msingi katika taaluma ya isimu.
Mawazo ya Chomsky yanadhirisha kuwa mbinu za uchanganuzii wa sentensi zilizotumika hapo awali hazikuwa toshelevu, kwani mbini hizo hazikuonesha tofauti kati ya muundo wa ndani na muundo wa nje wa sentensi.
Hivyo basi kwa ujumla sarufi geuzi zalishi hasa huchambua tungo kwa kuzingatia maana ya vijenzi vinavyounda sentensi fulani.
Mchango wa sarufi geuzi zalishi katika uchambuzi wa lugha ya Kiswahili.
(i)Sarufi Geuzi Zalishi (SGZ) inachanganua sentensi kwa kuzingatia umbo la nje na umbo la ndani katika sentensi ; Katika nadharia hii sentensi ina umbo la nje ambalo ndilo linajitokeza katika usemaji na hata inapoandikwa na umbo la ndani ambalo huwa limefichika na kujidhihirisha katika umbo jingine wakati wa kuongea (maana).Sarufi Geuzi Zalishi imeweza kuonesha uhuiano wa tungo ambazo zina umbo la nje tofauti na umbo la ndani sawa.
Kwa mfano;
(a)Makida anacheza mpira
(b)Mpira unachezwa na Makida
Mfanano wa tungo hizi umekitwa katika maana japokuwa sentensi “a” inaanza na Makida na “b” inaanza na mpira na mtendwa katika sentensi zote ni yuleyule na imebeba maana ile ile .Mchakato wa kubadili umbo la nje la sentensi “a” na kuwa “b’ umesababisha uchopekwaji wa kiunganishi “na” na kiambishi tendwa “w” katika kitenzi “cheza” hivyo kanuni geuzi tendwa ndiyo iliyotumika kuingiza mabadiliko hayo.
(ii)Sarufi Miundo Geuzi Zalishi imeweza kueleza utata wa sentensi kwa kuangalia maumbo yake ya ndani; hapa tunazungumaza utata wa kimuundo na maneno.
Kwa mfano ;
(a)Wanawake na watoto ishirini walikuja
(b)Wanawake idadi haijulikani, na watoto ishirini walikuja
©Wanawake kumi na watoto kumi walikuja
Sentensi zote hizi zinaelezea maana halisi iliyo katika sentensi kuuu . Inakua vigumu kwa anayesikia sentensi hiyo kujua msemaji anamaanisha nini lakini katika sarufi miundo geuzi zalishi wameweza kutuondolea utata katika maana za sentensi mbalimbali kwa kuonesha dhahiri hitaji la sentensi hiyo k wa msikiaji, ndio maana tukaweza kupata aina hizo tatu za sentensi zenye maana sahihi isiyo tata.
(iii)Sarufi Geuzi Zalishi wameweza kuonesha uhusiano uliopo baina ya sentensi zaidi ya moja zenye maumbo tofauti; kwamba katika sarufi geuzi zalishi wameweza kubainisha kuwa sentensi zinaweza kuwa na maumbo tofauti lakini zikawa na maana moja .
Kwa mfano;
(a) Malima amempiga Kingunge
(b) Kingunge amepigwa na Malima
Sentensi ya kwanza inasonesha kauli tendi na sentensi ya pili inaonesha kauli tendwa.Kuna uhusiano mkubwa kati ya sentensi ya kwanza na sentensi ya pili na uhusiano huu umeweza kuoneshwa dhahiri na sarufi miundo geuzi zalishi.Kwamba sentensi ya kwanza mtenda ni Malima na mtendwa ni Kingunge , pia katika sentensi ya mtendwa na mtendwa na ni wale wale. Hivyo kilichobadilika hapo ni umbp la sentensi lakini maana ni ileile.
(iv)Sarufi Miundo nGeuzi Zalishi wanaeleza na kuchanganua kinaganaga sentensi changamano; Hii ni kutoka na kuonesha vitenzi dhahiri katika sentensi changamano ambapo sarufi za nyuma zilishindwa kuonesha vitenzi hivyo na kuvifanya kama kishazi vumishi elezi .
Kwa mfano
(a) Mbuzi aliyepotea jana ameonekana asubuhi
(b) Kijana aliyekuja jana ameondoka leo
Katika sentensi hizi mbili maneno ‘aliyepotea ‘ na aliyekuja’ huonekana kama kitenzi, lakini katika sarufi za nyuma kabla ya sarufi miundo geuzi zalishi maneno hayo yalionekana kama kishazi vumishi.
Hivyo basi kwa ujumla tunaweza kusema kuwa sarufi geuzi zalishi imeleta mapinduzi makubwa sana katika uchambuzi na uchanganuziwa lugha kwa sababu sarufi geuzo zalishi imejikita katika maana ya maneno yanayoiunda tungo fulani, ambapo kwa kutumia kigezo hiki cha maana nduo maana wameweza kuichambua na kuifafanua sentensi changamano pia wameweza kuilezea tungo tata suala ambalo wanasarufi mapokeo na wanasarufi miundo virai hawakuliona kama lina umuhimu katika uchambuzi wa lugha kwani waljikita katika uhusiano wa vijenzi vya tungo.
Marejeleo
Kihore, Y.M na wenzanke (2012) Sarufi maumbo ya kiswahili Sanifu (SAMAKISA),Sekondari na vyuo Dar-es-salaam
Massamba , D.P.B. (2012) Sarufi miundo ya kiswahili Sanifu (SAMIKISA). Dar-es-salaam
Mdee, J.S (2007) Sarufi ya kiswahili sekondari na vyuo Dar-es-salaam; Dar-es-sallam University Press
Matinde, S. R. (2012) Dafina ya ligha isimu na Nadharia . Sekondari na vyuo .Mwanza ; Serengeti Educational Publishers.
|